NA-MWANDISHI WETU
Club ya Mazoezi ya Viungo Gombani Fitness imewajumuisha pamoja watoto mayatima 15 wananchama Wasiopungua 60 wa Club hiyo ,na vilabu vyengine maeneo mbali mbali kusini Na kaskazini Pemba Katika Iftaar Maalum iliyofanyika Katika Ukumbi wa ZRA Gombani Chake Chake ikiwa ni muendelezo na utaratibu unaofanywa na Club hiyo kila Mwaka.
Akizungumza mara baada ya ghafla ya iftar hiyo Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ahmed Abuubakar amewataka wana Club hiyo kuongeza bidii kuwafutarisha mayatima na wasiojiweza waliozunguka mitaani na katika jamii ili kuweza kujumuika nao pamoja ili mkusanyiko huo uweze kupata fadhila na ujira mkubwa Zaidi.
Amesema Fadhila na Hikma katika michanganyiko ya hairat inaweza kuongezeka mara dufu iwapo walengwa wakiwemo mayatima na wasiojiweza wataongezeka katika mkusanyiko huo mwaka ujao..
Aidha ameipongeza Gombani Fitness kwa kuona umuhimu wa kuftarisha ambapo pia ametumia fursa ya mkusanyiko huo kuwataka wananchi na vijana kuendelea Kudumisha amani iliyopo hususan kuelekea Uchaguzi.
Ahmed pia aliwataka wananchi kisiwani Pemba kuepuka kuwasema vibaya viongozi bila kuwafika wahusika yanapojitokeza matatizo mbali mbali ili waweze kuisaidiaPemba kwa pamoja kuzipatia ufumbuzi changamoto mbali mbali.
Hata hivyo amewaasa wananchi kisiwani humo Kuyatumia Majengo ya Serikali kama majengo ya kuzipatia ufumbuzi changamoto jamii na siyo kuyaogopa wanapopatwa na changamoto.
Aidha amewaasa Gombani fitness kuwashirikisha mapema katika mambo ya Hairat yanapojitokeza ili nguvu na mchango wa serikali uweze kuingia katika heri hizo.
Nae Mwenyekiti wa Club Hiyo Hamad Malengo amewaasa waumini wengine kuiga utaratibu huo ambao hauhitaji uwezo mkubwa kutimiza sunna hiyo ya kufutarisha watu mbali mbali.
Aidha amewakumbusha kuzisdisha bidii kufanya ibada zaidi katika mwezi huu wa Ramadhan.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo amewataka Wananchi na waalikwa hao kujiunga katika vikundi vya mazoezi ili kuimarisha Afya na miili yao.
0 Comments