Waziri wa zamani wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka amesema mzozo wa kibiashara kati ya Tanzania na Malawi kibao kitaigeukia Tanzania

Waziri wa zamani wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka amesema mzozo wa kibiashara kati ya Tanzania na Malawi licha ya Tanzania kuchokozwa na kujibu mapigo lakini kibao kitaigeukia Tanzania huku akisisitiza mazungumzo ya amani ni muhimu lasivyo Tanzania inaweza kupigwa faini kubwa kwasababu itaonekana imechukua sheria mkononi na kulipiza kisasi.

Prof. Tibaijuka kupitia ukurasa wake wa X amesema Malawi ni nchi isiyo na bahari kwa hiyo inalindwa na sheria za kimataifa kuhusu usafirishaji wa bidhaa kupitia nchi jirani kama Tanzania, mkataba wa WTO/GATT 1994: Ibara ya V – Uhuru wa Usafirishaji, inalinda haki ya nchi zisizo na bandari na kuzipa haki ya kupitisha bidhaa kupitia nchi jirani kwa njia bora zaidi na salama, bidhaa zinazopita hazipaswi kuzuiliwa au kucheleweshwa bila sababu ya msingi na bahati mbaya kulipiza hakuhesabiki hivo kama haukufuata utaratibu kisheria”

“Hairuhusiwi ubaguzi wowote unaopendelea bidhaa za nchi inayotoa njia ya kupita au nchi nyingine, hakuna ushuru au kodi ya forodha inayopaswa kutozwa bidhaa zilizoko njiani isipokuwa kwa gharama halali za kiutawala, maana  Tanzania hairuhusiwi kisheria  kuzuia au kuchelewesha bidhaa za Malawi kama njia ya kulipiza kisasi, ikiwa Tanzania ilikuwa na malalamiko, ilikuwa lazima ipitie utaratibu wa WTO, au SADC si hatua za upande mmoja, pili Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Sheria ya Bahari (UNCLOS), Sehemu ya X (Ibara 124–132) inalinda haki za nchi zisizo na bandari kwa nguvu”

“Pia Ibara ya 125, nchi zisizo na bandari zina haki ya kupitisha bidhaa zao kwa uhuru kupitia nchi jirani kwa kutumia aina yoyote ya usafiri, nchi jirani hazipaswi kuweka vizuizi visivyohitajika wala kudhoofisha usafirishaji huo, Malawi na Tanzania zote ni wanachama wa UNCLOS, hivyo haki hii ina nguvu ya kisheria ya kimataifa”

“Kabla ya kuhamia Nairobi kama Mkurugenzi wa UNHABITAT nilikuwa Mkurugenzi Mratibu wa maswala haya huko UNCTAD/WTO Geneva”

Kauli ya Tibaijuka inakuja siku moja tangi Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, itoe tamko la kupiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Nchi za Afrika Kusini na Malawi baada ya Nchi hizo mbili kuzuia mazao kutoka Tanzania.

Post a Comment

0 Comments