WANANCHI ZAIDI YA 112 WAPATIWA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA NA ZLSC SHEHIA YA UWANDANI


ZAIDI ya watu 112 wamejitokeza kupatiwa huduma ya msaada wakisheria na kituo cha huduma za Sheria Zanzibar(ZLSC) shehia ya Uwandani, wanawake ni 80 na wanaume 33. 
Hayo yameelezwa na afisa Miradi ZLSC Zanzibar Benny Louis Mlingi, wakati akitoa tathmini ya utoaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa shehia ya uwandani Wilaya ya Chake Chake.
Alisema wamelazimika kuchagua shehia ya uwandani, kwa kushirikiana na wasaidizi wa sheria wa Wilaya hiyo, kutokana na wananchi wengi wanahitaji huduma za msaada wa kisheria.
Aidha alisema mwamko ni mkubwa kwani wananchi wengi wamejitokeza kuhitaji huduma hiyo, na asilimia kubwa wanawake ndio wanaopata changamoto nyingi sana hata ukitizama idadi yao ni uthibitisho tosha wa hilo.
“Shehi ya Uwandani ni miongoni mwa shehia ambazo tumepata watu wengi, katika kambi hii ya utoaji wa elimu ya msaada wa kisheria ukilinganisha na shehia za Unguja,”alisema.
Afisa huyo alisema katika kambi hiyo wamegundua wanawake wengi hawana Vyeti vya Ndoa, vyeti vya kuzaliwa, ambapo wamekugundua kwamba ukosefui wa vyeti hivyo unawanyima wanawake haki zao.
Alifahamisha ukosefu wa haki hizo unapelekea wanawake kukosa mirathi, pamoja na haki za watoto wake endapo mmwenza wake atakapofariki, kitu ambacho kimepelekea mwamko kwa wanawake wengi hivi sasa kuanza kudai haki zao.  
Alisema katika suala la Vyeti vya Kuzaliwa, wengi wao changamoto yao ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kulipia, ikizingatiwa tayari umri nao umeshakuwa mkubwa, lakini utraratibu wa uombaji wanaufahamu.
Hata hivyo aliishauri serikali kupunguza gharama za ulipaji wa fedha za upatikanaji wav yeti hivyo, huku akiwataka wasaidizi wa sheria Wilaya ya Chake Chake kufika uwandani kuendelea kutoa elimu juu ya utoaji wa elimu ya msaada wakisheria.
Nae Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chiris Maina Peter, alisema wamegundua kuwa wananchi hawana vyeti vya kuzaliwa, ndoa, vitambulisho vya uzanzibari, NIDA na kitambulisho cha upigaji wa kura.
Alisema ipo haja ya kukutana na serikali kuweza kuzungumza nao juu ya upatikanaji wa nyaraka muhimu kwa wananchi, ikizingatiwa mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi.
Kwa upande wake msadizi wa sheria Jimbo la Ole Sada Hamadi Mbarouk, alisema wamegundua matataizo mengi ikiwemo ukosefu wav yeti muhimu ambazo ni jambo la msingi kwa mwananchi kuwa nazo.
Alisema tayari wamejifunza kuwa bado elimu inahitajika zaidi, kwa kuhakikisha taasisi yao watahakikisha wanaendelea kutoa elimu katika maeneo mbali mbali.
Nao wananchi waliopatiwa huduma hizo, wamepongeza ujio wa kituo cha ZLSC katika shehia yao na kuwapatia elimu ya msaada wakisheria, kwani umeweza kuwafumbua macho.
MWISHO

Post a Comment

0 Comments