Kampeni ya msaada wa kisheria kuja kusaidia kupungza migogoro katika jamii

Jaji mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdallah amesema kuwepo kwa kampeni ya msaada wa kisheria kunaweza kusaidia kupungza migogoro iliyopo katika jamii bila ya kufika mahakamani.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama samia iliyofanyika katika bustani za Mwanamashungu Mkoa wa Kusini Pemba, amesema  wazo la msaada wa kisheria linaweza kupunguza kesi kwa kiasi kikubwa  kufika katika mahakama kwani kesi nyingi zinaweza kutatuliwa endapo wananchi watapatiwa msaada wa kisheria.

Amesema kuwepo kwa sheria kunaweza kupatikana amani katika nchi hivyo ni vyema wananchi kuitumia kampeni ya mama katika kutatuliwa migogoro yao..
Katika hatua nyengine amesema serikali katika kuhakikisha inawaondoshea wananchi wake usumbufu sambamba na kuwasogezea huduma imejenga mahakama nne Pemba ambazo zitatumia mfumo wa teknolojia ya kisasa.
Naibu Waziri wa wizara ya katiba na sheria wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jumanne Abdalla Sigiri amesema mkakati wa kitaifa ya kampeni ya mama Samia ya mwaka 2023-2024 hadi mwaka 2025-2026 utekelezaji wa mkakati huo umeweza kushriki kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi hususan makundi maalumu ikiwemo wanawake, Watoto na watu wenye ulemavu.
 Kwa upande wake raisi wa chama cha wakili Zanzibar Joseph Magazi amesema msaada wa kisheria ni haki ya kila mmoja hivyo  kampeni hiyo italenga kutoa haki, usawa wa kijinsia na kuhakikisha hakuna anatakae baki nyuma katika kupata usaidizi wa kisheria. 

Akitoa salamu za mkoa Mkuu wa Mkoa kusini Pemba Rashid Hadidi Rashid kufanyika kwa kampeni hiyo katika mkoa huo kutachangia jamii kupata uwelewa juu ya msaada wa kisheria upatikanaji wa haki sawa na usawa wa kijinsia sambamba na kudumisha amani na utulivu.

Uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia iliyofanyika katika bustani ya mwanamashungi  ikiwa na lengo la kutoka msaada wa kisheria kwa wananchi ambapo kilele kinatarajiwa kufanyika tarehe 10/5/2025 katika Kijiji cha  mtende Wilaya ya kusini Mkoa wa kusini Unguja.

Post a Comment

0 Comments