WATAALAMU WA SHERIA WAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA SIKU 9 ZA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA PEMBA

NA-FATMA SULEIMAN-PEMBA
Wataalamu sheria wametakiwa kutumia lugha nzuri wakati wa kutoa  huduma kwa wananchi wenye matatizo mbali mbali yanayohitaji utatuzi wa kisheria Zanzibar.
 
Akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wadau wa msaada wa kisheria juu ya changamoto mbalimbali,mkuu wa wilaya ya Chake Chake Mgeni Khatib Yahya  kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia yaliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba.

Alisema Wataalamu wa sheria ni daraja kubwa kati yao na wananchi katika kuwasaidia kwenye masuala yao ya kisheria.

Aliwataka wanasheria hao kutokuwa sehemu ya watu wanaovunja sheria kwa kuwasaidia watu wanaovunja sheria kutokana na baadhi ya hukumu kutolewa yasiosahihi.

Alifahamisha kuna mambo mengi yanayofanyika ya uvunjifu wa sheria lakini baadhi ya kesi wananchi wamekuwa wakivunjika moyo kutokana na maamuzi yao.

"Ni matimaini yangu wasaidizi wa sheria wataisadia jamii juu ya changamoto mbalimbali za kisheria ", alieleza.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Chake Chake Mgeni Khatib Yahya alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni hiyo na watakapo fika maeneo husika kwa Wananchi watumie ujuzi wao na mafunzo waliopatiwa kwa kuwapatia huduma zilizobora wale wenye changamoto za kisheria.

Aliwataka wasaidizi wa sheria ambao wamepatiwa mafunzo hayo ya msaada wa kisheria wa mama Samia kutumia siku 9 za kampeni hiyo kutowa msaada wa kisheria wananchi wenye matatizo mbali mbali ikiwemo ndoa, Ardhi, Udhalilishaji nk.

Akizungumza mkurugenzi wa idara ya katiba na msaada wa kisheria Hanipha Ramadhan Saidi amesema kampeni ya mama samia lengo lake kuu ni kuhakikisha watanzania wote wanapatiwa huduma za msaada wa kisheria .

Amesema wananchi wengi wamekua wanakosa haki zao kutokana na kutokujua njia sahihi za kupita ili kupata haki zao hivyo waliamua kuja na kampeni hii ili kumkomboa mwananchi .
Kwa upande wake aaafisa mdhamini ofisi ya raisi katiba sheria utumishi na utawala bora Halima Khamis Ali amesema ni vyema kuyafanyia kazi kwa kina mafunzo ambayo wanapatiwa katika kuwapatia huduma sahihi wananchi ambao ndio walengwa katika kutatuliwa changamoto zao.

Ali Salum Hamad mkufunzi kutoka ofisi ya raisi katiba sheria utumishi na na utawa bora wakati akitoa elmu hio amesema wasaidizi wa sheria wana wajibu wa kufuata sheria na kanuni zilizowwekwa katika kuhakikisha wanamlinda mwanachi.

Post a Comment

0 Comments