NA-FATMA SULEIMAN PEMBA
Wanawake wa vyama tofauti kisiwani pemba wavilalamikia vyama kuwanyima ruzuku yakufanya kamapeni majimboni
Wanawake hao wameyasema hayo walipokuwa wakizungumza na habari hizi kwa nyakati tofauti
Ambapo wamesema kukosekana kwa ruzuku hizo kumechangia kwakiasi kikubwa kutokufikiwa kwa sera zao ipasavyo
Licha ya juhudi wanazozichukuwa katika kutafuta nafasi za uongozi lakini bado wanakumbwa na changamoto ya ukosefu wa fedha zakuendesha kampeni zao
Aidha wamesema licha yakuendeleza kampeni za nyumba kwa nyumba kutokana na uhaba wa fedha katika kuwaomba kura wananchi lakini bado wanakumbana na changamoto ya uzalilishaji kwa kutolewa maneno machafu wakati wakuomba kura
Akizungumza Asha Saidi Suleiman mgombea wa uwakilishi jimbo lamtambile kutoka chama cha Ada tadea amesema changamoto hiyo imemfanya kutokufikia malengo yakutangaza sera zake kwa weledi
Nae Asha Siasa Ame mgombea uwakilishi mupitia chama cha CUF ameeleza kuwa mapambano yake yakutafuta kura yalikuwa ni makubwa lakini ukosefu wa fedha ulipunguza nguvu yakupiga kampeni majimboni
Wakizungumzia wasemaji wa vyama tofauti akiwemo Katibu wa chama cha CUF Moh'd Haji Kombo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo kutokana na sababu vyama vingi mwaka 2020 kukosa uwakilishi katika bunge nakupelekea kukosa ruzuku na hivyo imepelekea chama chao kuwa na uhaba wa fedha zakuendesha kampeni
Akizungumza Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa Habari Tanzania Zanzibar TAMWA ZANZ Mzuri Issa anasema wanawake ni kundi maalum ambalo Kwa miaka mingi limerejeshwa nyuma, hivyo lazima vyama viwe na sera ya kijinsia na kutekelezwa Kwa vitendo.
Anasema Moja katika jambo muhimu ni kuwatambuwa wale wanawake wanaoweza kuwa viongozi na kuwapa nafasi na mashirikiano ya Hali na mali ili kuweza kutekeleza.
"Sasa kama hawajapata ni bahati mbaya na ni mapungufu makubwa Kwa vyama vya Siasa kwani tuliwaambia mapema Kwa vile vyama ambavyo vinapata ruzuku waweke fungu maalum na Kwa vile ambavyo havipati waanze kutafuta fedha mapema ili wanawake wasipate shida"alisema.
0 Comments