Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mdhamini wa Wizara ya Kazi na Uwekezaji kaimu mkuu wa Idara utumishi na uendeshaji Said Saleh Mohammed katika Ukumbi wa Wizara hiyo Gombani Chake Chake Pemba.
Amesema, lengo la kutoa elimu kwa waandishi wa habari ni kupata uelewa wa dhana ya uwepo wa Idara ya PPP katika shughuli za uwekezaji ikiwemo kijamii na kiuchumi.
Akiwasilisha mada ya dhana mzima ya Idara ya mashirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi Mratib wa Idara hiyo Machano Mmanga Mgeni amesema, Idara hiyo imejikita katika uwekezaji wa umma ambao ni taasisi za Serikali katika kutengeza miradi ya Serikali, uwekezaji wa kibinafsi ambao unatokana na mtu au taasisi isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kuwekeza pamoja katika uwekezaji wa umma na binafsi.
Akizungumzia faida zinazotokana na taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kupunguza shinikizo la ufadhili kwa Serikali, upatikanaji wa pesa za kufanyia miradi ya Serikali kwa wakati kupitia sekta binafsi.
Ameongeza, pia ukuaji wa uwekezaji juchangia ajira na kuleta maendeleo ya miundombinu, huduma bora na upatikanaji wa teknologia inayoendana na wakati.
Mratibu huyo pia ametaja baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa na Idara ya PPP ni pamoja na Elimu, ujenzi wa Barabara, ujenzi wa viwanja vya ndege na nyenginezo.
Nae Mwandishi zuwena Shabani kutoka ZBC TV amesema, mafunzo hayo yamewasaidia kuitambua Idara hiyo na kufahamu namna ya miradi wanayoitekeleza, hivyo watatumia kalamu zao ili kutoa ufafanuzi kwa yale miradi ambayo inatekelezwa na Idara hiyo kwa lengo la kuendeleza uchumi wa nchi.
Mashirikiano Baina ya sekta ya Umma na binafsi ni mkataba wa muda mrefu kati ya sekta binafsi na taasisi ya Serikali kwa ajili ya kutoa mali au huduma ya umma, ambapo sekta binafsi hubeba sehemu kubwa ya hatari na wajibu wa usimamizi na malipo yake huhusishwa na kiwango cha utendaji kazi.
0 Comments