TAMWA YAWAFUNZA WAANDISHI JUU YA UDHALILISHAJI

Na,Tatu Juma 

Waandishi wa habari wametakiwa kubadili mitazamo ya jamii juu ya matukio ya udhalilishaji kwa wanawake na wasichana.




Wito huo umetolewa na Mwanachama mkonge wa chama  cha Waandishi wa habari wanawake Tamwa Zanzibar bi Haura Shamte alipokua akiendesha mafunzo ya udhalilishaji dhidi ya wanawake na wasichana huko Tamwa Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema vitendo vya udahlilishaji kwa wanawake na wasichana kila kukisha vinachukua mstari wa mbele na kupelekea kupunguza kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini.


Licha ya hayo amewataka waandishi kuibua matatizo mbali mbali yanayowakumba  wanawake ikiwemo udhalilishaji wa mauwaji, kingono pamoja na vitisho.


Nae Afsa mradi huo Asia Hakimu amesema kuwa lengo kubwa la mradi huo ni kutoa elimu kwa waandishi wa habari pamoja na vitengo vyengine kwa lengo la kupunguza matukio ya udhalilishaji nchini hususani maeneo ya Kaskazini A na B Unguja na Pemba.


Wakichangia mada miongoni mwa wanamafunzo hayo wamesema kuwa sasa ipo haja ya kushikana mikono kwa pamoja ili kusaidia jamii dhidi ya vitendo hivyo sambamba na kutafuta njia mbadala ya kukinga kadhia hiyo.

Mwisho 

Post a Comment

0 Comments