HUYU HAPA SAMIA WA PEMBA Zawadi Amour Nasor:Mwanamke shupavu asieogopa kushindana na wanaume


Aomba Ridhaa ya Kuwakilisha Wananchi wa Jimbo la Konde
NA-AFARA MAKAME-PEMBA 
Katika harakati za kuelekea uchaguzi mkuu, jina la Zawadi Amour Nasor limezidi kuvuma miongoni mwa wananchi wa Jimbo la Konde, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Akiwa ni miongoni mwa wanawake wachache waliopata uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya uwakilishi , Zawadi anaingia katika kinyang'anyiro hiki akiwa na dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya kwa jamii anayoitumikia.

Historia na Maisha ya Awali
Zawadi Amour Nasor alizaliwa na kulelewa katika kijiji cha kiuyu kwa manda kilichopo Konde karibu na maeneo ya msitu wa ngezi , akiwa mtoto wa kwanza familia yenye maadili na heshima kwa jamii. Alipitia elimu yake ya msingi na sekondari konde na utaani zilizopo ndani ya Pemba, kabla ya kujiendeleza kitaaluma katika fani ya uongozi wa jamii na maendeleo. Tangu akiwa mdogo, alikuwa akionesha ujasiri, msimamo na kujitoa kwa ajili ya kusaidia wenzake, hasa wanawake na watoto.
Uzoefu na Uongozi
Safari yake ya uongozi mgombea huyo ilianza kama mwanachama wa chama cha mapinduzi mwaka 1997 
Na baada yahapo alianza kushika nafasi ya mjumbe wa kamati ya jimbo 
Mwaka 2018-2019 kushika nafasi ya mjumbe wa mikakati ya ushindi  
Hadi mwaka 2020 aliingia katika kinyang'anyiro cha mgombea uwakilishi jimbo la konde nafasi ambayo ilimpa ushindi  wakidedea ndani ya jimbo hilo 
Ambapo kupitia nafasi hiyo aliteuliwa kuwa naibu waziri wizara ya maji nishati na madini nafasi ambayo anaendelea nayo hadi sasa.


NJE YA SIASA 
Zawadi ni  mke nani mama wa watoto saba,
Licha yakuwa na majukumu yakifamilia amekuwa mstari wa mbele katika shughuli za kijamii na harakati za maendeleo kwa muda mrefu.

 Amehudumu katika serekali akiwa kama Mwalimu katika skuli mbili ikiwemo makangale na konde msingi na pia taasisi zisizo za kiserikali zinazohamasisha haki za wanawake,ikiwemo shirika la CARE INTERNATIONAL Pamoja na elimu kwa watoto wa kike, na mazingira

 Amejijengea heshima si tu kwa wanachama wa CCM bali hata kwa watu wa kada mbalimbali kutokana na uadilifu wake na uwezo wa kusikiliza na kushughulikia matatizo ya watu.

Mbali na hayo zawadi ni mtu wa dini na imani mana wengine humuita ustadhati kwamuonekano wake wakujigubika kwa nguo za stara hata kuungana na jumuiya za kidini kuendeleza mustakabali wa maisha ya dini 

Dira na Malengo  
Akizungumza kuhusu azma yake ya kugombea nafasi ya uwakilishi, Zawadi anasema:  
"Nina ndoto ya kuona Konde inapata mwakilishi anayesikiliza wananchi wake, anayesukuma maendeleo ya kweli na anayewajali wote bila ubaguzi wa jinsia wala nafasi."

Zawadi ameonesha ujasiri wa kipekee kwa kupambana wanaume wengi , vikwazombali mbali ikiwemo ubaguzi wa kijinsia kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi ni mama wa nyumban  , udini ,kutengana na familia yake kutokana na nyadhifa hizo lakini ameo nesha ushupavu na kuyashinda yote hayo huku akiweka vipaumbele vyake ambapo moja wapo ni -  
- Kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia vikundi vya uzalishaji.  
- Kukuza ajira kwa vijana kupitia kilimo, uvuvi na ujasiriamali. Huku kaulimbiu yake ikisema  "Kazi na utu tunasonga mbele!"  
Kauli hii inaakisi dhamira yake ya kuwakilisha kwa vitendo, si kwa maneno tu.

Mapokezi ya Wananchi
Katika mikutano na matembezi yake, Zawadi amepokelewa kwa hamasa kubwa, hasa na wanawake na vijana ambao wamekuwa wakihamasika kwa kuona mmoja wao anasimama kuwatetea. Ushirikiano alio nao na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa ni wa kuridhisha, jambo linaloongeza nguvu katika kampeni zake.

Hitimisho  
Zawadi Amour Nasor ni mfano halisi wa mwanamke jasiri, na ni miongoni mwa wanawake walioingia Katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini Tanzania,ambao  wameonyesha ushiriki wao katika kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ambapo Kwa upande wa Zanzibar, jumla ya wanawake 855 walichukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za ubunge, uwakilishi, na udiwani akiwemo Bi Zawadi ambae ni mwanamke mwenye dira, anayetamani kuona Konde inainuka kielimu, kiafya na kiuchumi. Na anaehitaji kupata ridhaa ya kuwa mwakilishi wao ili awe daraja la kuwasogeza kwenye maendeleo ya kweli kupitia Ilani ya CCM.

Post a Comment

0 Comments