Makala: Asha Said Suleiman – Mwanamke Jasiri Alieingia katika kinyanganyiro cha Uongozi.


(Mitazamo yakijamii kuwa siasa ni ya wanaume,mifumo dume ndani ya jamii
Ukosefu wa fedha wakuendeshea kampeni havikumvunja moyo kusimama imara kusaka nafasi ya kugombea uwakilishi.)
Mwanamke wa Leo ni Sauti ya Maendeleo ya Kesho
NA-AFARA MAKAME ABASS
Ni katika mazingira haya ndipo tunamshuhudia Asha Said Suleiman , mwanamke mwenye ujasiri ambaye ameingia kwenye kinyang’anyiro cha uongozi, licha ya changamoto na mitazamo hasi inayowakumba wanawake wengi.

 Kupitia safari yake ya kisiasa anawakilisha ndoto za wanawake wengi waliodhulumiwa kimya kimya, na sasa wanataka kusikika.

Kauli mbiu yake ni wazi: “Mwanamke wa leo ni Maendeleo yakesho"
Kwani Mwanawake ni nguzo muhimu katika kupigania masuala ya uongozi na maendeleo ambayo yanajumuisha masuala ya kiuchumi, kiutamaduni na hata  kisiasa pia huleta mtazamo wa huruma na  mshikamano ambapo mwanamke anaendelea kuwa kiungo muhimu katika jamii.

Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na sheria mbali mbali za Tanzania zilizopitishwa na bunge zinamtambua mwamake kama ni kiongozi Jasiri na mkakamavu, mpambanaji na anaweza kuongoza katika ngazi mbali mbali za uongozi kama vile siasa. 

Aidha jamii inamchukulia mwanamke kama ni mama na kiongozi katika familia jambo ambalo linamfanya kumuongezea ujasiri wa kupambania nafasi mbalimbali za uongozi.

Katika kizazi hiki cha mabadiliko, wanawake wengi wamejitokeza kwa ujasiri kuchukua nafasi katika uongozi na maendeleo ya kisiasa  akiwemo Asha Said Suleiman, mwanamke mwenye dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu, hususan kupitia uongozi wa kijamii na kisiasa ambapo asha alionesha toka hapo awali kua hahitaji tuu kuwa kiongozi wa familia pekee bali anahitaji kuwa nguzo muhimu ya uongozi wa taifa katika kuleta maendeleo, jambo hili linadhihirika wazi kupitia mwanamke  huyu Jasiri ambae anagombea nafasi ya uakilishi Chama Cha Ada Tadea .
  Taarifa Fupi
 Asha Said Suleiman  amezaliwa mwaka 1976 katika Kijiji cha msingini Pemba akiwa ni miongoni mwa watoto waliokua na ujasiri na wenye uthubutu toka akiwa mdogo katika familia yake Aliweza kujipatia elimu yake ya msingi katika skuli ya Michakaini Pemba ambapo elimu ya sekondari alisoma skuli ya Hamamni iliyopo Unguja Zanzibar Asha alianza kujihusisha na siasa miaka ya hivi karibuni na ilipofika mwa 2015 akaamua kuingia kwenye kinyanganyiro cha kugombea kupitia chama cha  ADA-TADEA  na hadi sasa dhamira yake ni ile ile ambapo kwa sasa anawania nafasi ya Uakilishi katika Jimbo la Mtambile  ambalo halijawahi kumsimamisha mgombea mwanamke.

Safari ya Uongozi
Asha Said Suleiman ni mfano wa mwanamke aliyeinuka kutoka katika changamoto za maisha ya kawaida hadi kuwa sauti ya matumaini kwa jamii yake. Kwa miaka mingi, amekuwa mstari wa mbele kushiriki katika masuala ya maendeleo ya kijamii, hasa kwa kushirikiana na vikundi vya wanawake, wajasiriamali wadogo na vijana.

Kwa kugombea Jimbo la Mtambile, Asha ameonyesha kwamba mwanamke ana uwezo na haki ya kushiriki katika maamuzi ya kisiasa, kutunga sera, na kusimamia rasilimali za jamii kwa haki na uwazi. 
Kauli Mbiu Yake
Mwanamke wa leo ni sauti ya maendeleo ya kesho.”
Changamoto Alizokutana Nazo
Changamoto katika nafasi za uongozi ni moja ya kikwazo kinachowakwamisha wanawake mbalimbali katika kufikia malengo yao ya kuwa viongozi ambapo miongoni mwa hizo  ni Mitazamo ya kijamii kuwa siasa ni ya wanaume, ukosefu wa rasilimali za kifedha kwa ajili ya kampeni, Kupambana na mfumo dume ndani ya jamii na taasisi ambapo yote hayo ni changamoto za wazi ambazo anaendelea kukumbana nazo hadi sasa.
Wito kwa Wananchi
“Ni wakati wetu sasa. Tuwe sehemu ya mabadiliko kwa kumpa nafasi mwanamke, si kwa sababu ni mwanamke tu, bali kwa sababu ana uwezo.” nakupitia sera sheria mikataba tunaweza kuona nijinsi gani mwanamke anaweza kushiriki katika masuala kama.haya 

Kama Katiba ya Zanzibar ya 1984, kwenye kifungu cha 11 na cha 14, vimeweka wazi kuwa kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu.

  Aidha Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2050 imeelezea jinsi gani masuala ya usawa wa jinsia juu ya kuondoa unyanyasaji na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake.

Napia kwa sera ya jinsia inaeleza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya utoaji maamuzi,

 Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC)  ambayo mkataba wake ulitiwa saini mwaka 2008 inaeleza, kutaka kuondoa utafauti na kuwatenga wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kusaidia kuwepo usawa wa kijinsia katika nchi wanachama na kufikia asilimia 50/50 kwenye  maamuzi.

Mkataba wa kimataifa wa kutokomeza aina zote za ubaguzi, (CEDAW) wa mwaka 1979
 Ibara ya 12,  inasisitiza ushiriki sawa wanawake na wanaume kufikia asilimia 50/50 kwenye nyanja za maamuzi, serikalini na taasisi binafsi.

Ingawa bado wanawake wanaendela kukumbana na changamoto lakini Licha ya hayo, Asha ameendelea kusimama imara, akiwa na imani kwamba mwanamke anapopewa nafasi, anaweza kufanya zaidi ya matarajio ya jamii.

Asha Said Suleiman ni mfano halisi wa mwanamke kiongozi wa kizazi kipya ambaeni jasiri, mkomavu, mwenye maono na aliyejitoa kwa ajili ya jamii yake aliye tayari kuongoza kwa uadilifu na maono. Kupitia ADA-TADEA, anaamini anaweza kuleta mabadiliko ya kweli katika Jimbo la Mtambile na kuwa sauti ya matumaini kwa wanawake wengine waliokata tamaa ya kugombea, Kupitia uongozi wake, anawaonesha wanawake wengine kuwa si tu wanaweza, bali wanapaswa kuwa sehemu ya maamuzi makubwa yanayoathiri maisha yao.

"Kumwinua mwanamke ni kuiinua jamii nzima."

Post a Comment

0 Comments