Mkurugenzi akabidhi Baskeli 30 kwa wanafunzi wa elimu mbadala Kaskazini A Unguja.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada tu yakumalizika hafla hiyo amesema miongoni mwa mikakati ya Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania na Zanzibar ni kuisaidia jamii kielimu hivyo kwa sasa imeamua kuwapa elimu watoto pamoja na vijana waliokata masomo kwa kuwapa ujuzi mbali mbali ili kuweza kujikwamua kimaisha.

Nae Afsa Wilaya Kaskazini A Ungunja ndugu Juma Mwadini Abdallah amesema ingawa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali inajitahidi kutoa muamko lakini Wilaya hiyo ipo katika mazingira ya utalii na baadhi ya vijiji bado wazazi hawana muamko kwa watoto wao juu kuwafichua na kuweza kupata elimu.
Amesema kuwa kwasasa wamefanikiwa kwakiasi kikubwa kupitia programu mbalimbali kwa kuzunguka ndani ya shehia tofauti Wilayani humo na hatimaye kuwaibua vijana walioacha masomo na sasa wameweza kupata masomo na mafunzo madhubuti.
Kwaupande wake mwanafunzi aliyejiunga na elimu hiyo Jamila Omar Muhammed mkaazi wa Chaani Juwakuu amesema kuwa amepata manufaa makubwa baada ya kujiunga na darasa hilo kwani kwasasa anauwezo wakusoma nakuandika kwa ufasaha zaidi pamoja na kupata ujuzi wa masuala ya ujasiri amali.
Amesema kutokana na elimu anayoipata darasani hapo matarajio yake ya baadae nikujiajiri na hatimaye kuweza kupata kipato chake cha halali.
Mradi huu unaotambulika kwa jina la Daraja umeshirikisha tume ya Taifa Tanzania bara uliolenga maeneo matatu ikiwemo Masasi,Geita na Zanzibar ambapo kwa hapa Unguja umeanzia Kaskazini A Unguja ambao unalengo la kuinua jamii kielimu na kimaisha.
0 Comments