Waandishi wa habari Pemba wametakiwa kuibua na kufuatilia changamoto zinazosababisha udhalilishaji katika maeneo mbalimbali ambayo sio maarufu ili kuongeza mapambano dhidi ya vitendo hivyo .
Akizungumza katika mafunzo ya siku mbili na waandishi wa habari yaliyofanyika katika Ofisi za TAMWA -Pemba Afisa Program kutoka TAMWA -Zanz Asia Hakim amesema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza vitendo hivyo na athari zitokanazo na udhalilishaji kwa wanawake na wasichana kwa kuelimisha jamii kwani vyombo vya habari vinasikika na jamii mzima.
Amesema mradi huo umejikita zaidi katika mikoa ya kaskazini Unguja na Kaskazini Pemba kwani takmwimu zimeonesha waathirika wengi wa maeneeo hayo hawana muamko wa kuripoti matukio hayo licha ya kufikiwa kielimu.
Aidha amesema Ipo haja kwa waandishi wa habari kuelekeza nguvu zao ili kuhakikisha jamii wanakua na muamko wa kuripoti na kudai haki pindi wanapofanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Kwa upande wake muasilishaji Haji Nassor Mohammed, amesema miongoni mwa vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na wasichana ni pamoja na usafirishaji haramu wa binaadamu, kwani vitendo hivi huengezeka kutokana na ukosefu wa elimu na maadili kwa jamii.
Amesema waandishi wana jukumu la kutumia kalamu zao kuelimisha jamii kutambua vitendo vya udhalilishaji vinavyoharibu maisha ya wanawake na wasichana.
Nao washiriki wa mafunzo hayo Mwamize mohammed amesema mafunzo hayo yatawasaidia katika majukumu yao kwani watatumia kalamu zao kuelimisha jamii juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea kutokea kwenye jamii.
Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa "Tunaweza Pamoja" unaotekelezwa ma UN Women kwa kushirikiana na TAMWA Zanzibar kwa ufadhili wa Serikali ya Norway chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa unaolenga kujenga jamii salama dhidi ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na wasichana.
0 Comments