Familia ya mtoto aliyekatwa mkono Z'bar yataka Rais Mwinyi aingilie kati.

Na Tatu Juma Zanzibar,

Familia ya mtoto aliyekatwa mkono yamlilia Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali  Mwinyi yadai haki na stahiki ya mtoto wao.

Akizungumza na mwandishi wa habari za mitandaoni mama mzazi wa mtoto huyo Safia Said Omar anauyetambululika kwa jina la Said Abdallah Khamis huko nyumbani kwao Kijichi Kikaangoni Wilaya ya Magharib A Unguja.

Amesema kuwa chanzo cha kadhia hiyo  kwa mtoto wake alikua anapatiwa matibabu ya tumbo na badae kuekewa kenyula mkononi, kitendo ambacho kilipelekea kukwamisha mshipa wa damu na kuharibika kwa mkono na hatimaye kusababisha kukatwa.

Mama huyo ameishukuru Serikali ya Mapibduzi ya Zanzibar kwa kuwaunga mkono kwa kupata rufaa ya kwenda kupata huduma ya  matibabu kwa kuelekea Hospitali ya Muhimbili, jijini Dar-esalam na hatimae mtoto huyo kupona lakini kwa sasa anaulemavu wa ukosefu wa mkono mmoja.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa amedai kuwa changamoto iliyopo kwa sasa familia hiyo imechukua hatua ya kufuatilia stahiki za mtoto huyo za kiserekali lakini bado hakuna msaada mwengine wowote baada ya kumalizika kwa matibabu kwa mtoto huyo.

"Sasa hivi tunaishi na mazingira magumu mtoto wangu amekua mlemamavu, tunamuomba Mh.Rais atusaidie kwasababu inauma mtoto kuwa mzima halafu akasababishiwa kuwa na ulemavu,"amesema mama wa mtoto huyo.

Nae Baba mzazi wa mtoto huyo Abdallah Khamis Ali amesema kuwa tatizo liliopo sasa ni kutofahamu wizara ya Afya inamipango gani madhubuti kuhusiana na kadhia hiyo.

"Sisi walituita wakatwambia kwamba tufanye majadiliano, lakini sisi tukawambia hatuwezi kufanya majadiliano kwasababu sisi hatujapata ripoti kutoka Wizara ya Afya, kwaiyo hatuwezi kufanya majadiliano kutoka kwenu. kwanza tujue kama sisi wazazi ripoti imendeleaje ndipo tukae sasa"


"Tukaamua sasa kutafuta wanasheria, tumefanya jitihada kubwa kwaiyo tunamuomba muhesmiwa Rais atusaidie hususan sisi wanyonge ambao hatuna hatapakuenda ili mtoto aendelee kupata haki yake"amesema Baba mzazi wa mtoto Said

Kwaupande wake Waziri wa maendeleleo ya jamii Jinsia na Watoto Mhe  Anna Athanas Paul amefahamisha kuwa kwa sasa Wizara hiyo ipo katika mchakato wa kutafuta bima ya Afya ya Mtoto huyo katika kipindi chote cha makuzi yake hadi kufikia umri wa miaka 18.

"Sisi kama Serikali tumelibeba jambo hili kuhakikisha kwamba mtoto huyu hapati changamoto nyengine yeyote baaada ya hii aliyokuwa nayo"amesema Mhe. Anna

Mbali na hayo pia nae Katibu mtendaji wa baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar Ussi Khamis Debe amesema kuwa kwaupande wao wataendelea kufanya ukaribu na mtoto huyo kuhakikisha anakuwa vizuri na kuishi pasipo na mazingira magumu.

"Kijana wetu kukatwa mkono sio mwisho wa maisha kwamba tutaendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu wa kijana huyu kuhakikiaha kwamba anakuwa,akifikia miaka mitano, saba tunaweza kuona anaweza kutumia vifaa gani saidizi atakapokuwa tutampatia mkono bandia ambao utamsaidia kupunguza ule ukakli wa shuhuli zake za kila siku"amesema Katibu Ussi.

Kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar namba 8 ya mwaka 2022 kifungu namba 30 kinasema kuwa kila mtu anawajibu wa kutekeleza,kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu ukijumuisha kutoa taarifa zinazohusiana na uvunjwaji wa haki hizi.

Na kifungu 31(1) kinaeleza kuwa watu wenye ulemavu hawatobaguliwa au kudhalilishwa kwa namna yeyote ile na katika ngazi yeyote kutokana na sababu ya ulemavu wao.

Post a Comment

0 Comments