Jumla ya matukio 138 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Julai, 2026 ambapo waathirika walikuwa 138. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 118 sawa na asilimia 85.5), wakifuatiwa na wanawake 19 (asilimia 13.8) na mwanaume alikuwa mmoja (1) sawa na asilimia 0.7.
Idadi ya matukio ya udhalilishaji kwa mwezi yamepungua kwa asilimia 3.5 kufikia matukio 138 kwa mwezi Julai, 2026 ikilinganishwa na matukio 143 yaliyoripotiwa mwezi wa Juni, 2026. Matukio yaliyoripotiwa kuongezeka kwa mwezi Julai, 2026 yalikuwa kutupa watoto, kulawiti/kunajisi, kutorosha, na shambulio la aibu/kukashifu.
Idadi ya matukio ya udhalilishaji kwa mwaka yameongezeka kwa asilimia 29.0 na kufikia matukio 138 kwa mwezi Julai, 2026 kutoka matukio 107 yaliyoripotiwa mwezi wa Julai, 2025. Matukio mengi yameripotiwa kuongezeka kwa mwezi Julai, 2026 isipokuwa matukio ya wizi wa watoto.
Wilaya zinaongoza kwa Matukio ya Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia Julai, 2026
Wilaya ya Magharibi ‘A’ imeripotiwa kuwa na matukio mengi (matukio 32) zikifuatia Wilaya ya Mjini na Magharibi ‘B’ ambapo kumeripotiwa matukio 24 kwa kila wilaya. Wilaya ya Kusini na Mkoani zimeripotiwa kuwa na idadi ndogo ya matukio(matukio 4 kwa kila wilaya).
Wilaya ya Magharibi ‘A’ imeripotiwa kuwa na idadi kubwa ya matukio ya kubaka ikilinganishwa na wilaya nyengine, ambapo jumla ya matukio ya kubaka 17 sawa na asilimia 27.4 ya matukio yote ya kubaka.
Kati ya matukio 62 ya kubaka yalioripotiwa kwa mwezi wa Julai, 2026, matukio manne (4) sawa na asilimia 6.5 yameripotiwa kwa wanawake na matukio 58 yameripotiwa kwa wasichana sawa na asilimia 93.5.
Aina ya Matukio ya Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia na Hatua Zilizochukuliwa Julai, 2026 Matukio 117 kati ya matukio 138 yaliyoripotiwa yapo chini ya upelelezi wa Jeshi la Polisi sawa na asilimia 84.8 ya matukio yote yaliyoripotiwa, aidha matukio 17 yamepelekwa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (asilimia 12.3) na matukio manne (4) yamefungwa na polisi (asilimia 2.9).
Takwimu za udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu, Julai 2026
Jumla ya waathirika watatu (3) wenye ulemavu wamefanyiwa ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa mwezi wa Julai 2026. Ambapo wanawake walikuwa wawili (2) na mvulana mmoja (1) ambao wote walikuwa na ulemavu wa akili.
Muathirika wa wa ubakaji alikuwa mmoja (1), kulawiti alikuwa mmoja(1) na shambuluo la aibu/kukashifu mmoja(1).
Idadi ya Makosa na Mashauri Yaliyofunguliwa kwa Mkoa Julai, 2026
Kati ya mashauri 40 yaliyofunguliwa katika Mahkama za udhalilishaji Zanzibar, mashauri 38 bado yanaendelea sawa na asilimia 95.0 na mashauri mawili(2) yametiwa hatiani sawa na asilimia 5.0.
0 Comments