Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi[CCM] Taifa,chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi imekutana katika kikao chake maalum,kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui,Zanzibar Jumapili tarehe 19 Mei 2024.
Pamoja na mambo mengine,Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Ndugu Khamis Yussuf Mussa [PELE] kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Kwahani,Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliopangwa kufanyika tarehe 8 Juni 2024 kufuatia kifo cha aliyekua mbunge wa jimbo hilo,Ndugu Ahmada Yahya Abdulwakil SHAA aliefariki dunia tarehe 8 April 2024.
Vile vile Kamati Kuu kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa [NEC] imefanya uteuzi wa Ndugu Suzan Peter Kunambi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania [UWT].
Aidha Kamati Kuu ya CCM,imezipongeza Serikali zake zote mbili SMT inayoongozwa na Dkt.SAMIA SULUHU HASSAN na SMZ chini ya Dkt.HUSSEIN ALI MWINYI kwa namna zinavyoendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.
0 Comments