Kamati za mazingira zilizopo katika mashehia kisiwani Pemba zimetakiwa kuielimisha jamii juu ya masuala ya haki yanayotokana na tabia nchi ili kurekebisha athari za mabadiliko hayo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa mwanvuli wa asasi za kiraiya Zanzibar Hassan Khamis Juma katika hafla ya kujengewa uwelewa wanakamati hao juu ya masuala ya haki yanayotokana na tabia nchi huko madungu chake chake Pemba.
Amesema ikiwa dunia ipo katika janga la mabadiliko ya tabia nchi ni vyema wananchi kwa kushirikiana na kamati kuchanganua haki zao ili kuweza kupata mbinu za kupunguza madhara yanayojitokeza
Kwa upande wake Mwalimu Khamis Mwalimu kutoka idara ya mazingira Pemba amesema ni vyema kamati za shehia kuitunza na kuilinda miundombinu iliyowekwa katika shehia zao ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
Naibu katibu wa mwenvuli wa asasi za kiraiya Pemba Alawi Bakari amesema maeneo mengi Tanzania yameshaharibika kutokana na mabadiliko ya labia nchi hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja katika kuibua hoja, haki na wajibu kwa wanachi na kubuni miradi mbali mbali ili kuyarudisha baadhi ya maeneo yalioharibika na athari hizo .
Wakizungumza kwa niaba ya washiriki hao mara baada ya kupatiwa mafùnzo ya haki na wajibu katika mabadiliko ya tabia nchi Muhammed Hassan Abdallah na Asha Hamad Ali wamesema kuwa mafunzo hayo watayafanyia kazi kwa vitendo kwa kuyafikisha katika shehia zao sambamba na kutumia namna bora za kuhifadhi mazingira kwa maendeo ya sasa na vizazi vijavyo.
Wamesema athari za mabadiliko ya tabia nchi hupelekea kukosa kufanya shughuli nyingi za kibinaadamu kutokana na maeneo mengi kisiwani pemba kuharibika ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa maeneo ya kilimo, ukame , mafuriko , ongezeko la nyuzijoto kuzidi ambapo athari hizo huathiri jamii na nchi nzima kwa ujumla .
Wamesema licha ya jitihada mbali mbali ambazo wamekua wakichukua katika kukabiliana na athari hizo kama kupiga matuta kupanda miti lakini bado hazijazaa matunda ukilinganisha na athari zilizopo.
0 Comments