WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAMESISITIZWA JUU YA KUFUATA MAMRISHO YA ALLAH

Waumini wa dini ya kiislamu wamesisitizwa juu ya muhimu wa kufuata miongozo ya Qur ani kwa vile imeweka njia sahihi ya maisha ya mwanadamu .
Hayo yameelezwa na mwakilishi wa jimbo la ole ambae pia ni waziri wa nchi ofisi ya raisi tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum ya SMZ Mh Masoud Ali Mohd mara baada ya kumalizika mashindano ya kuhifadhisha Qur an huko ole chake chake Pemba. 
Amesema kuwa Qur an imekuja na muongozo tosha katika maisha ya wanaadam hivyo ni vyema walezi kuvishijihisha na vizazi vyao ili kukua katika misingi mema .
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya chake chake Ali Mohd Chande  amewapongeza walimu wa madrsa kwa namna wanavyowaendeleza watoto katika misingi inayotakiwa katika dini .
Katika mashindano hayo zaidi ya wanafunzi 130 kutoka jimbo la ole na majimbo mengine, walioshiriki mashindano  hayo kuanzia juzuu moja hadi 30 ambayo yameandaliwa na jumuiya0 ya kuhifadhisha Qur ilipo ole dodo, wamepatiwa zawadi na mwakilishi huyo ikiwa ni mwendelezo wa kuyadhamini mashindano  ndani ya jimbo hilo kwa miaka mitatu sasa.

Post a Comment

0 Comments