Mwakilishi wa jimbo la Ziwani Suleiman Makame Ali amewataka walimu wazazi na walezi kuwa na mashirikiano ya pamoja katika kuwahifadhisha kitabu cha kur an ili kuwawekea muongozo mwema wa maisha yao ya baadae .
Ameyasmea hayo huko katika Skuli ya msingi Dk philip mpango iliopo kwale jimbo la ziwani chake chake pemba.
Kwa upande wake Sheha wa shehia ya kwale Khamis Suleiman Ali amesema kuwa wazazi wana jukumu la kuwaelekeza watoto katika masuala ya dini .
Akisoma risala ya mashindano hayo Katibu wa jumuia ya maendeleo ya walimu wa madrsa jimbo la ziwani Harith Suleiman amesema Kur an ni msingi wa haki katika maisha ya mwanaadam hivyo kumuomba mwakilishi kuendelea kuwaunga mkono katika masuala ya dini .
Aidha amewaomba viongozi kuwekeza katika masuala ya dini ili kupata radhi kutoka kwa Allah .
Mashindano hayo yalioandaliwa na jumuiya ya kuhifadhisha Qur an jimbo la ziwani yamezishirikisha zaidi ya madrasa 70 ambapo yamezinduliwa kwa mara ya kwanza ndani ya jimbo hilo lengo ilikiwa ni kuwajengea watoto wa kiislamu miongozo mema na kuwaepusha na vikundi viovu
0 Comments