Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara katika kujiepusha na maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi ili kujiondoa na hatari ya kupoteza maisha endapo watashindwa kupata huduma mapema.
Hayo yameelezwa na Daktari wa maradhi ya saratani Pemba Katib Shaame Khatib wakati akitoa maelezo juu ya ugonjwa huo kwa wahariri wa vyombo mbali mbali kisiwani humo .
Akitoa takwimu za saratani amesema makadirio yaliotolewa na Shirika la kimataifa la utafiti wa saratani la IARC ambalo ni Shirika la tanzu la WHO yalitokana na utafiti wa nchi 185 yakionesha kuwa idadi kubwa ya nchi zilizoshiriki hazitengi fedha za kutosha kuhudimia wagonjwa wa saratani si mpango wa afya kwa wote au UHC.
Amesema mwaka 2022 kulikuweko na wagonjwa wapya wa saratani milioni 20 na kati yao milioni 9.7 walifariki dunia na waliobaki hai ambapo waliobaki hai miaka mitano baada ya kubainika na saratani ni milioni 53.5.
Mratibu wa tume ya ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar amesema wahariri na waandishi wa habari wanajukumu la kuelimisha jamii juu ya maradhi hayo sambamba na kuwahimiza kupima saratani ya shingo ya kizazi ili kuwaepusha na athari amabazo zinaweza kuwapata .
Aidha amesema ni vyema akina baba kuwahimiza akina mama kuwa na utaratibu wa kwenda kupima sambamba na kuacha njia ambazo zimekatazwa moja wapo ikiwa ni kufanya mapenzi katika umri mdogo ili kujikinga na ugonjwa huo .
Khadija Kombo ambae ni muhariri wa Zbc Pemba na Saidi Omar muhariri wa radio jamii Mkoani wameupongeza uongozi wa chama cha waandishi wa habari Tanzania Tamwa Zanzibar kwa kuwapatia Mafunzo wahariri kwani awali ilikua hawana uwelewa wakutosha juu ya ugonjwa huo .
Nao Bakari Mussa Juma Muhariri wa Gazeti za Zanzibar leo na Ali Masoud Kombo muhariri wa radio jamii micheweni walisema kuwa ugonjwa huo umekua tishio kutokana na takwimu zilizotolewa ipo haja kwa vyombo vyote vya habari kuendelea kushirikiana na taasisi husika ili jamii iweze kupata uwelewa na ugonjwa huo .
0 Comments