Imeandikwa na Tatu Juma – Zanzibar
Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA-ZANZIBAR) kimewataka wanawake kushiriki katika kugombania nafasi mbali mbali kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 2025.
Akizungumza na wandishi wa habar Mkurugenz wa chama hicho dokta Mzuri Issa,katika ofisi za TAMWA-ZANZIBAR mkoa wa kusini unguja,amesema kuwa ipo haja ya wanawake kuwa mstari wa mbele kwa kuwania nafasi katika uchaguzi wa mwaka huu ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii.
Akieleza kuwa katiba ya jamuhuri ya muungano ya mwaka 2024 kifungu namba 10 imempa nafasi ya kipekee mwanamke kushiriki katika siasa na kumlinda dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na kuimarisha haki na usawa kwa pande zote.
Na kwa upande wake mhadhiri kutoka chuo kikuu cha dar es salam Dkt William John,amefahamisha kuwa suala la kujiamin, kijilinda,na kujithamini ni muhimu sana kwa mwanamke ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji hususa kwa wagombea na wasimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo ,wadau na wanaharakati katika masuala ya kijamii wakisititiza kuepuka vurugu katika uchaguzi huo na kuwa na umoja na mshikamano ili kuimarisha amani na utulivu katika jamii.
Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya haraka iwapo watasimama na kijidhatiti katika kugombania nyadhifa tofauti bila ya kuyumbishwa , kukatishwa tamaa na kuleta mafanikio makubwa nchini.
0 Comments