ATCL yazindua safari Pemba hadi Tanzani bara Prf: Mnyaa atoa yamoyoni

WAZIRI wa Uchukuzi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Prf: Makame Mbarawa Mnyaa, amesema kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania ‘ATCL’ kisiwani Pemba, ni eneo jingine la kukifungua kisiwa cha Pemba, kiuchumi, kama ilivyokuwa ahadi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ameyasema hayo jana, kwenye uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo, hafla liyofanyika uwanja wa ndege wa Pemba na kusema zitaanzia baina ya kisiwa cha Pemba, Unguja na Tanzania bara.

Amesema ATCL, sasa litawarahisishia zaidi wananchi wa Pemba, wakiwemo wafanyabiashara, kufika safari zao kwa wakati, ikiwa ni hatua muhimu ya kufikia ndoto zao.

Ameeleza kuwa, kuwa ndege hiyo itafanya safari zake mara tatu kwa siku ikiwemo Jumanne, Ijumaa na Jumapili na zitachukuwa abiria kati ya 76 na nyingine 50.

"Niwatake wananchi wa Pemba, muitumie ndege hii kutokana ubora na na umadhubuti wake na uhakika wa safari zake za kuanzia, hapa Pemba, Unguja, Dar-es Saalan na mikoa mingina kadhaa ya Tanzania," alieleza.

Amefafaniua kuwa, ndege hiyo imekuja baada ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi kwa viongozi wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari

Aidha, Waziri huyo alipongeza hatua ya serikali ya kuona sasa inatanua mbawa zake kwa shirika hilo la ndege, jambo linalokuza pato la nchi.

kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la ndege Tanzania Peter Ulanga, amesema kupitia shirika hilo, mwezi Machi mwaka huu, ilizindua safari katika mikoa ya Mtwara na Iringa na kupitia mji Kinshasha ya Kidemokrasia ya Congo.

Amesema safari hizo ziliweza kupokekewa vizuri sokoni humo, na zaidi ya abiria 320 hutumia Air Tanzania, katika safari zao, wastani wa abiria 370 wakitokea upande wa mkoa wa Mtwara na 500 kwa DR. Congo kila wiki katika vituo hivyo sambamba na kusema kuwa kupitia shirika hilo, wanajivunia mno, kuwepo kwa ndege mpya 15, ambazo zinafanya kazi, pamoja na ile m oja maalum kwa ajili ya mizigo.

"Niwajuikishe kuwa katika ndege hizo, saba zimenunuliwa na serikali ya Jamuhuri ya awanu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia, jambo linalotutoa ari ya kufanyakazi kwa bidii na hamasa,"alieleza.

Mkuu wa wilaya ya Chake chake Mgeni Khatib Yahya amesema, Pemba ni kisiwa cha kikubwa cha kihistoria cha utalii kinachounganisha kivutio cha kiuchumi kama vile fukwe.

AmeisemaPemba imeweza kufunguka kiuchumi na kuunganishwa sehemu mbali mbali, kutoka nje ya nchi na ndani ya kisiwa cha Zanzibar, jambo ambalo kuja kwa ndege hiyo ni hatua nyingine.

"Tunamshukuru sana Rais wa Zanzibari kuwa kukifungua Pemba kiuchumi tena kwa vitendo, kutokana na usafiri wetu wa anga, utaweza kurahisisha na uchumi kukua kw kasi," alifafanua.

Ilifahamika kuwa, kampuni hiyo, imefanikiwa kuongeza miinuko, kutoka 20 kwa siku hadi 140 kwa wiki, katika maeno mbali ya ndani ya nje na kuweza kuiunganisha Tanzania na dunia.

Shirika la Ndege la Tanzania ATCL, lilianzishwa rasmi Novemba mwaka 2002, chini ya sheria ya Makampuni ya Tanzania, ambapo lilichukua majukumu ya shirika la zamani la ndege la Tanzania, ATC.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni ATCL linamiliki ndege 16, ikiwemo aina ya Bombardier Dash 8 Q400, Bombardier CS300 (Airbus A220-300) na Boeing 787 Dreamliner.

Post a Comment

0 Comments