FATMA SULEIMAN PEMBA
Afisa Mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali amesema wizara ya Afya Pemba imejipanga katika kusimamia mikakati madhubuti juu ya malezi ,makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto
Ameyasema hayo huko wizara ya afya Chake Chake Pemba wakati akizungumza na Waandishi na kusema kuwa Wizara ina jukumu la kuwalinda na kuwakuza watoto ili kukua katika mazingira salama
Alieleza kusema kuwa wananchi wanapaswa kutumia lishe bora ikiwemo mboga mboga ambazo zinapatikana kwa urahisi ili kujenga taifa lenye afya njema na ukuaji wa mtoto
Alifahamisha kuwa kuna hatua mbalimbali ambazo wizara ya afya Pemba imezichukuwa katika kuhakikisha watoto wanapata malezi makuzi ya awali ikiwemo kuweka mazingira rafiki katika vituo vya afya katika kuwachanja watoto, kutoa elimu kwa jamii
Alieleza kuwa mjengeko wa kinga za mwili za mtoto unaanza kutokana na kunyonya maziwa ya mama hivyo ni jukumu la akina baba kulisimamia hilo ili kumkuza mtoto katika mazingira salama.
"Tunatamani watoto wote wanaozaliwa Zanzibar wanabakia wakiwa na misingi mila silka sambamba na malezi makuzi na Maendeleo ya awali ya afya bora", alieleza.
Hata hivyo kwa upande wake daktari dhamana wilaya ya Chake Chake Dk, Sharif Hamad Khatib alisema kuna umuhimu kwa akina mama kuwa natabia ya kuchanja chanjo zinazowahusu pale tu wanapojingundua ni wajawazito katika kuona wanamkinga mtoto mapema na kumuepusha na magonjwa mbalimbali ikiwemo pepopunda TT , Ttanus Toxoid, chanjo ya donda koo kifaduro.
0 Comments