Wito huo umetolewa na Mkufunzi na mtaalamu kutoka shirika la Children in cross-fire Devis Alexander Gisuka yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Jamirex iliyopo Mwenge jijini Dar esalam.
Gisuka amesema miaka ya awali ya mtoto kuanzia siku 0 hadi miaka miwili ni kipindi muhimu ambapo hukua kwa kasi kimwili , kiakili ,kihisia na afya yake ya sasa na baadae huimarika endapo wazazi watazingatia malezi na makuzi yake ya awali.
Amesema malezi yenye muitikio mkubwa ,upendo , afya bora , chanjo za msingi ,lishe bora , ulinzi na usalama wa mtoto , fursa ya kujifunza mapema ni mambo muhimu yanayochangia afya njema na makuzi ya mtoto na kumtengenezea maisha bora ya sasa na baadae.
Akizungumza mtaalamu wa malezi na makuzi ya awali ya mtoto kutoka katika taasisi ya Mdarasa Childhood Sharifa Suleiman Majid amesema malezi yenye upendo, ufuatiliaji wa afya pia huchangia kwa kiasi kikubwa ukuwaji wa haraka mtoto hivyo ni vyema waandishi kutumia kalamu zao katika kuibua changamoto zilizopo ndani ya jamii ili maendeleo ya kisera na kisheria yaweze kupataikana na kumfanya mtoto akikuwa kwenye mazingira salama.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Rais ya ufuatiliaji, utendaji Serekalini (ZPDB) DK Ibrahim Bystike Kabole amesema kwa sasa ni jukumu la waandishi wa habari kuwaelimisha wazazi na walezi katika kuwa na juhudi na kuhakikisha watoto wanapata vyakula vyenye virutubisho ili kuongeza ufanisi na ukuaji kwa lengo la kuwa na afya njema na jamii yote iliobadilika katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto.
Mkurugenzi wa muungano wa klabu ya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya amesema ni muhimu waandishi wa habari kuwa vinara na kuhakikisha wanaibadilisha jamii juu ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto ili ili kujenga jamii bora ya sasa na baadae.
Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Zuhura Juma na Ramadhan Singamo wamesema watahakikisha elimu walioipata inafika ipasavyo ndani ya jamii ili kuleta mabadiliko na mtoto aweze kupata malezi na makuzi ya awali.
Mafunzo hayo ya siku nne kwa waandishi wa habari Zanzibar ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto yaliowashirikisha maafisa wa wizara ya afya na watendaji wa clabu ya waandishi wa habari Tanzania yenye lengo la utekelezaji wa Programu shirikishi ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto inayojumuisha taasisi za binafsi na za serekali inayosimamiwa na Taasisi ya Rais Ufuatiliaji na Utendaji Serekalini (ZPDB)
0 Comments