Billion 28, zawafikia wakulima wa Karafuu kisiwani Pemba



FATMA SULEIMAN, PEMBA

Zaidi ya Bilioni Ishirini na nane zimelipwa na Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC)  kwa  wakulima wa zao la karafuu kisiwani Pemba kuanzia tarehe 1 Julai  hadi tarehe 14 September 2025.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar (ZSTC) Soud Said Ali katika kikao cha majadiliano huko Samael Chake Chake Pemba, amesema kupitia huduma za Mix by Yas wameweza kuwalipa wakulima Bilioni kumi na sita milioni mia sita sitini  na mbili.

Alieleza fedha nyengine kati ya hizo zimelipwa kwa njia ya Benk na fedha mkononi kwa vile mara nyengine hulazimika  kulipwa kwa njia tofauti ikiwemo huduma za kibenki  na huduma ya Mix by Yas ili kuwarahisishia wakulima sambamba na waepusha na majanga mbali mbali.

Alisema kuwa ni vyema wananchi wote kuendelea kushajihishana ili wakulima kuendelea kuitumia huduma ya Mix by Yas na kunufaika nayo kwani ni njia rahisi na sahihi kwa kupokelea fedha zao.

‘’ Niwaombe Wakulima wa Zao la Karafuu endeleeni kupokea malipo kwa njia ya Simu ya Mkononi (MIX by YAS) kwani ni rahisi na sahihi na salama kwa upokeaji wa fedha zenu’’, alifahamisha.

Akizungumza katika kiako hicho Meneja wa Mix by Yas Zanzibar Azizi Saidi Ali amesema katika kipindi cha miaka mitano wakulima elfu kumi na nne( 14,000)  na mawakala elfu ishirini na tano ( 25,000) ambapo zaidi ya wakulima elfu moja ( 1000) waliwahudumia katika huduma yao kwa kipindi hichi cha miezi kadhaa toka huduma hii kuboreshwa.
Alieleza kupitia zao la karafuu uchumi wa Pemba umeendeelea kupanda kwa kasi na kubadilisha maisha ya watu wake kwa vile wananchi wamekuwa wakipata fedha kupitia zao hilo .
Hata hivyo alilipongeza Shirika la ZSTC kwa kwa kusimamia vyema na kuendelea kufanya maboresho ya huduma zao katika kuwainua kiuchumi wananchi wa Pemba.

‘’ Nalipongeza Shirika la ZSTC kwa kusimamia vyema maboresho ya huduma
katika kuhakikisha wananchi wanafaidika na zao hili’’, alisema.

Nao baadhi ya watendaji wa Shirika la ZSTC wakielezea baadhi ya changamoto walisema ni vyema Mix by Yas kuboresha huduma zao ili kuona wanarahisisha na kuwavutia zaidi wakulima.
Walieleza baadhi ya huduma za usajili wa laini zimekuwa kikwazo hivyo
kuomba kurekebisha ili suala la fedha za wakulima liweze kuwa jepesi na kufikiwa na huduma katika wakati husika.

Katika hatua nyengine waliupongeza uongozi huo kwa kuona ipo haja ya kuwakutanisha na kutatuwa changamoto zilizopo ili huduma ziweze kuwa bora kwa wakulima na kuongeza pato la nchi.
Kikao hicho cha majadiliano kuhusiana na mfumo, ambacho kimewashirikisha watendaji wa Shirika la ZSTC na watendaji wa huduma za Mix by Yas kilichofanyika Samael Chake Chake Pemba kikiwa na lengo
la kuongeza kasi ya utekelezaji na kukuza uchumi wa Pemba.

Post a Comment

0 Comments