WANUFAIKA WA MRADI WA SWIL PEMBA WADHIHIRISHA FURAHA YAO MBELE YA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA

WANUFAIKA  mradi wa  SWIL Kisiwani Pemba  wamepongeza mashirikiano mema yanayoendelea kufanywa na ubalozi wa  Norway, nchini Tanzania katika kutatua changamoto zinazowakabili  wanawake ili kuweza kuufikia usawa wa kijinsia  na kuweza kushiriki katika nafasi za Uongozi ngazi mbalimbali.
Wakitoa pongezi hizo kwa nyakati  tofauti katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TAMWA kwa upande wa Pemba wanufaika hao wakiwemo,wanawake wagombea vyama mbalimbali, waandishi na, wahariri vyombo mbalimbali vya habari,wananchi maeneo tofauti, walionufaika  kupitia ufadhili wa Norway nchini Tanzania ambao wanaendelea kufadhili mradi wa kuwawezesha wanawake kuwa viongozi SWIL unaotekelezwa na TAMWA ZNZ  ,PEGAO, JUWAUZA na ZAFELA.
Wamesema  mradi  huo wa SWIL  chini ya ufadhil wa Norway Tanzania umegusa jamii moja kwa  moja hususan ni wanawake katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizokuwa zinawakabili katika kufikia ndoto zao za kushiriki katika uongozi.
Akisimulia  mabadiliko aliyoyapta  kupitia mradi huo Katija  Mbarouk  Ali ,amesema awali  alikosa utayari katika kushiriki katika mchakato wa kutafuta nafasi ya uongozi hususan katika majimbo ,lakini kupitia mradi huo aliweza kujitolea ,kujiamini na kuongeza uthubutu kuwania nafasi hiyo licha ya kushindwa  kutokana na sababu zilizopo katika michakato ndani ya  vyama  pamoja ,na mitazamo ya wanajamii.

Wakiwa katika mkutano  wakutoa ushuhuda akiwemo Halima Suleiman Kombo,  Hasina Omar Salim, Tatu Abdalla Msellem na Maryam Hemed Said wameuomba ubalozi wa Norway kuendelea kuwaunga tena mkono ili kufanya kazi kubwa Zaidi ya kuwasaidia wanawake kufikia nafasi za Uongozi.
Kwa upande wandishi na wahariri wa vyombo vya habari kutoka gazeti la Zanzibar leo kisiwani Pemba Radio  jamii   Mkoani pamoja na radio jamii Micheweni  akiwemo Ali Massoud kombo,Bakar Mussa Juma, pamoja na Amina Massoud Jabir  wamesema elimu iliyoitolewa   kupitia mradi huo  wamenufaika  katika kuisaidia jamii kuthamini mchango wa wanawake ,kuandika habari zenye kuitetea jamii ya wanawake,kuanzisha madawati ya kijinsia katika vyombo vyao,kubadilika nafasi za  juu za uongozi katika vyombo vyaom  kupata vitendea kazi pamoja  na fedha .
Awali akizngumza na wanufaika hao Balozi wa Norway nchini Tanzania  Tone Tinnes  amewataka watekelezaji wa mradi huo wa SWIL  kisiwani pemba ambao ni TAMWA ZNZ pamoja na PEGAO ,kuendeleza juhudi hizo  za kuwasaidia wanawake katika kufikia usawa wa kijinsia bila kukata tamaa kutokana na changamoto zinzorudisha nyuma ,kwani juhudi za kuufikia usawa  huo zinahitaji  uvumilivu .
Ameongeza kuwa ili kuweza kuufikia utajiri wa usawa wa kijinsia kama uliofikiwa  na nchi ya Norway ni lazima  kuendeleza juhudi hizo bila kukatishwa tamaa na changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbali mbali.

 Kwa nyakati tofauti   mkurugenzi wa TAMWA  ZNZ  Mzuri Issa Ali amewashukuru wanufaika hao  katika kuendeleza  mashirikiano mema ya utekelezaji wa mradi ,ambapo amewaasa kuendeleza mashirikiano hayo  ili kuweza kuufikia usawa wa kijinsia .
Ziara hiyo maalum  ya siku tatu kutoka kwa ubalozi wa Norway Tanzania  kuonana kuzungumza na wanufaika wa mradi wa SWIL unguja na Pemba  nchini,ilianza katika kisiwa cha Unguja ikiwa ni ufuatiliaji wa mradi wa SWIL.
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments