DK MWINYI AKISHIRIKI ZOEZI LA KUPIGA KURA AFURAHISHWA NA HALI YA UTULIVY NA AMANI ZANZIBAR


Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi ameeleza kufarijika na Hali ya Amani na Utulivu iliotawala katika Vituo vya Kupigia Kura na Nchi nzima kwa Ujumla .
Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba 2025 baada ya kupiga kura katika Shehia ya Kahani Jimbo la Kwahani ,Kituo Cha Karikaoo Majira ya Saa 2:25 asubuhi akiambatana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi .

Mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi amefahamisha kuwa kuwepo kwa hali ya Utulivu kunatoa fursa pana ya Wananchi kujitokeza kwa Wingi kupiga kura na kutimiza wajibu wao Kikatiba na kidemokrasia.

Aidha amewapongeza Wagombea wengine wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kwa kuendesha kampeni za Kistaarabu muda wote wa Kampeni hatua alioielezea kuwa ni kuimarika kwa Demokrasia hapa Nchini.

Akielezea Matumaini yake juu ya Uchaguzi amesema Chama Cha Mapinduzi kina matarajio makubwa ya Ushindi kufuatia Utekelezaji wa Mafaniko wa Ilani yake ya 2020-2025 na Mambo makubwa ya Kimaendeleo ilioyatekeleza katika nyanja mbalimbali. 

Dkt, Mwinyi ameipongeza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa Maandalizi mazuri ya Uchaguzi na kuwasisitiza Wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua Viongozi wanaowataka.

Vyama 11 vya Siasa vimesimamisha Wagombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa 2025. 

Post a Comment

0 Comments