Wasichana wawili wenye waliofahamika kwa majina ya Ruwaiha Mmanga Omar na Ruwaida Mmanga Omar wenye umri wa miaka 12, wakaazi wa Kwale Mpona wanasoma darasa la tano katika Skuli ya Kizimbani iliyopo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, wamekutwa wameshafariki dunia wakiwa wananing’inia kwenye mti ikisadikiwa kuwa wamejinyonga.

Tukio hilo limetoka jana Novemba 17.2025 saa 4 za asubuhi katika eneo la Kwale Mpona Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba mara baada ya wananchi kuwaona watoto hao wakining’ininia kwenye mti aina ya Mkeshia.

Chanzo hasa cha tukio Hilo hakijafahamika ingawa inasemekana kuwa watoto hao watumwa na mama yao kufanya kazi za ndani ndipo walipoamua kuchukua uamuzi huo wa kujinyonga.

Mwandishi wa Habari hizi alichukua hujudi za kufuatilia tukio hilo kwa kutaka kuzungumza na wazazi wa wasichana hao lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na hali ya wazazi hao kugubikwa na ombwe la huzuni.n

Daktari wa kitengo Cha dhamana Hospital ya Kinyasini Said Ali, amesema uchunguzi umeonesha chanzo cha watoto hao kupeteza maisha ni baada ya kukosa kupumua huku akitoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kuwa karibu na watoto hasa pale wanapo katika mazingira ya kawaida.

Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Timothy Mwampaghale, amethibitisha tukio hilo ambapo amesema kuwa chanzo cha tukio hilo ni watoto hao kulazimishwa kufanya kazi za nyumbani ndipo walipo ondoka nyumbani na kwenda kujinyonga.

Aidha Kamanda Timothy, amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo

Mjadala mkali umeibuka miongoni mwa wananchi kutokana na mazingira ya tukio hilo kwa kile kinachodhaniwa kuwa wasichana hao wamenyongwa badala ya kujinyonga kwani katika mazingira ya kawaida mtu hawezi kujinyonga huku miguu yake ikiwa na uwezo wa kusimama kwenye Ardhi sambamba na urefu wa mti waliojinyongea kuwa mrefu kiasi kwamba kuweza kupanda juu kwa watoto hao sio rahisi.

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wanaendelea kufuatilia kwa kuzungumza Jeshi la Polisi wazazi, ndugu na majirani wa marehemu hao ili kufahamu chanzo halisi cha tukio hilo.