Kuanzishwa madawati ya jinsia katika vyuo ni kuwawezesha Wanafunzi kurupoti kesi na kufanyiwa kazi kwa haraka.



Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Anna Athanas Paul amesema Lengo la kuanzishwa madawati ya jinsia katika vyuo ni kuwawezesha Wanafunzi kurupoti kesi na kufanyiwa kazi kwa haraka.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wapya wa mwaka 2025-2026 katika Chuo kikuu Cha Zanzibar (Zanzibar university) huko Tunguu Mkoa wa kusini unguja 

Aidha Mhe. Paul amewataka kuwa makini na kurupoti vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wakati kunapotokea ili wahusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria.

Hata hivyo Mhe. Anna amekiagiza chuo hicho, kutenga Bajeti maalum kwa ajili ya Dawati hilo, ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliokusudiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto Siti Abasi Ali amesema Chuo hicho, kinapotokea Wanafunzi wenye silka na Tamaduni za Mzanzibar.

Hivyo wameamua kufanya kikao hicho ili waweze kuungana pamoja katika kupiga vita vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji vinavyoendelea Nchini.

Nao Wanafunzi WA chuo hicho, wameahidi kuitumia dawati Hilo kwa ajili ya kurupoti kesi wakati zinapotokea ili kuviondosha vitendo hivyo.

Dawati la jinsia katika chuo kikuu Cha Zanzibar ZU, limeanzishwa mwaka 2022 ambapo tayari nimeshapokea jumla ya Kesi 5.

Post a Comment

0 Comments