WANANCHI WA PUJINI DODO WATAKIWA KUDUMISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025



NA-ARAFA ABASS PEMBA 
UONGOZI WA  wa Shehia ya Dodo,Pujini Wilaya ya Mkoani mkoa Kusibi Pemba 
Umewataka wananchi  wa shehia hiyo kuendelea kudumisha Amani  iliyopo na kuepukana na vishawishi vitakavyopelekea uvunjifu wa amani na kupelekea madhara kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na  Ridhiwani Assa Omar sheha wa Shehia hiyo ya Dodo pujini  alipikuwa akizungumza na wananchi Katika mkutanowake  maalum na  wananchi ndani ya shehia hiyo wenye lengo kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani kuelekea Uchaguzi mkuu 0ctobar 29   mwaka huu.
Akmesisitiza kuwa uongozi wa shehia hiyo  hautokubali kuona mwananchi  yeyote anavuruga amani katika shehia hiyi  kwani madhara yake ni makubwa zaidi  iwapo itatokea kutetereka na waathirika wakubwa zaidi ni wanawake watoto pamoja n na wazee.
 
Sheha Ridhwan   amewataka wazazi na walezi kuwaelekeza vijana wao kutokaa makundi makundi kwani itapeleka kuzungumza maneno yasiyo na msingi nakupelekea kushiriki katika vitendo vya uvunjifu wa amani .

" baadhi ya Makundi makundi ambayo yamekuwa wakikaa vijana  tayari yameanza kuonesha ishara mbaya ikiwemo kulenga mawe,na kutoa maneno ya kashfa kwa magari ya vyombo vya ulinzi na usalama na wakishafanya hivyo hukimbilia mabondeni hii siyo ishara nzuri kwaio naomba  wazazi  nao muendelee kuwakanya watoto hususan ni vijana kuacha mara moja tabia  hizo ili kuendelea kutawala amani katika shehia hiyo.
 
Kwa upande wake Afisa Mkaguzi wa Shehia ya Dodo  Ali Juma Abdulla amesema kuwa  Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kukabiliana na aina yoyote ya vurugu na tayari limejikita katika kulinda amani na wala sio  kuwatisha wananchi .
 " kwakupiga doria Maeneo mbali mbali sisi jeshi la polisi tayari tumeshajipanga lengo za hizo doria ni kuhakikisha amani na usalama unakuwepo wakati huu kuelekea uchaguzi ndani na hata baada ya uchaguzi kwahiyo wananchi wajibu wenu ni amani tuendelee kuidumisha ba hifu ya doria za Askari. 

Aidha Mkaguzi huyo ametoa  wito kwa jamii kushirikiana na viongozi wa shehia na jeshi la polisi kuripoti dalili zozote za uvunjifu wa amani ili hatua  zichukuliwe mapema kabla amani haijatoeka na kupelekea madhara kwa wananchi na taifa.

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo akiwemo Abdillah Juma Khamis Amesema wataufanyia kazi ushauri huo sambamba na kufikisha ujumbe  kwa jamii ili nchi ibaki kuwa salama ndani ya kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya Uchaguzi kwa maendeleo ya wananchi.

Post a Comment

0 Comments