Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitapata ushindi wa kishindo katika Mikoa ya Pemba kutokana na kazi kubwa na nzuri ya kufanya Kampeni inayofanywa na Viongozi wa Chama na Jumuiya zake hususani UWT kuanzia ngazi ya Matawi, Wadi, Majimbo, Wilaya na Mikoa.
Kufanya kampeni za kistadi, kupita nyumba kwa nyumba na kuelezea kazi za maendeleo zilizofanywa na Serikali za CCM katika kipindi cha mwaka 2020-2025,pamoja na kuinadi Ilani mpya ya 2020-2030, ambapo wananchi wa Kisiwa cha Pemba wameonesha muitikio mkubwa wa kuiunga mkono CCM hivyo Ushindi wa Kishindo ni mweupe kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Siku ya Jumatano Oktoba 29.A
Makamu Zainab ameeleza hayo leo tarehe 19 Oktoba, 2025 katika Kikao na Viongozi wa UWT wa Matawi ya Jimbo la Chonga, Kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kukutana na Viongozi wa UWT katika Mikoa ya Zanzibar.
0 Comments