Katika miaka ya hivi karibuni, kisiwa cha Pemba kimekumbwa na ongezeko la matumizi ya dawa za kupanga uzazi za dharura, maarufu kama P2, hasa miongoni mwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 25.
Wengi wao hutumia dawa hizi kama njia ya kawaida ya kujikinga na mimba, bila kuelewa madhara yake kiafya na kijamii.
P2 ni nini? P2 ni dawa ya homoni aina ya levonorgestrel inayotumika kuzuia mimba endapo itatumiwa ndani ya saa 72 baada ya tendo la ndoa bila kinga. Hata hivyo, wataalamu wa afya wanabainisha kuwa dawa hii inapaswa kutumika mara chache tu, kwa dharura, si kama njia ya kawaida ya uzazi wa mpango.
Sababu za Ongezeko la Matumizi
Kuna sababu kadhaa zinazopelekea vijana wa kike kutumia P2 kupita kiasi. Kwanza, uelewa mdogo wa elimu ya afya ya uzazi miongoni mwa vijana. Pili, woga wa kwenda kliniki au kuomba ushauri kwa hofu ya kuhukumiwa. Tatu, upatikanaji rahisi wa dawa katika maduka bila usimamizi wa kitaalamu. Nne, ushawishi wa mitandao ya kijamii na marafiki wanaodai kuwa P2 haina madhara.
Athari kwa Afya na jamii
Madaktari wanatahadharisha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya P2 yanaweza kusababisha: mzunguko wa hedhi usio wa kawaida, kichefuchefu, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, mabadiliko ya homoni na matatizo ya uzazi kwa muda mrefu. Kijamii, matumizi haya yamechangia kuongezeka kwa tabia za ngono zisizo salama, pamoja na magonjwa ya zinaa.
Elimu kwa jamii
Elimu ya afya ya uzazi ni muhimu, pamoja na kuanzisha vituo rafiki kwa vijana vinavyotoa ushauri kwa usiri. Serikali kupitia Wizara ya Afya inapaswa kudhibiti uuzaji holela wa dawa za dharura, huku wazazi wakihimizwa kuzungumza kwa uwazi na watoto wao kuhusu afya ya uzazi. Pia, vijana wahamasishwe kutumia njia salama kama kondomu au vidonge vya kawaida vinavyosimamiwa kitaalamu.
Maoni ya wataalamu ambae ni Afisa uzazi salama kitengo shirikishi afya ya uzazi na mtoto Pemba Kauthar Abdallah Juma pamoja na Fatma Hassan Khamis ambae ni msimamizi wa wa vituo vya huduma rafiki kwa vijana Pemba walisema 'P2 si dawa ya matumizi ya kila mara. Inapotumiwa kupita kiasi, inaweza kuathiri viwango vya homoni mwilini na kuharibu mzunguko wa hedhi. Vijana wanapaswa kupata elimu sahihi kabla ya kutumia dawa hizi.'
Njia za kupunguza tatizo
Hatua ya kwanza ni kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kupitia shule, vyuo, na vikundi vya kijamii. Vituo rafiki vya vijana vinapaswa kuanzishwa ili kutoa ushauri bila kuhukumu. Serikali inapaswa kudhibiti uuzaji holela wa dawa za dharura na kuhakikisha wauzaji wanatoa maelezo sahihi kwa wateja. Wazazi pia wanayo nafasi kubwa katika malezi ya watoto wao. Mazungumzo ya wazi kuhusu masuala ya kijinsia na uzazi ni muhimu. Kukwepa mada hizi hakutaleta suluhisho; badala yake, kunawaacha vijana kutafuta majibu mitandaoni ambako mara nyingi wanapotoshwa.
Chama cha waandishi wa Habari Tanzania Zanzibar TAMWA ZANZ nao ni wadau wakubwa katika kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia kwa kina juu ya afya ya uzazi salama kwa wasichana kupitia mradi wake wa afya ya uzazi kwa uzazi salama (SRHR) ambapo imekua ikichukua hatua mbali mbali katika kuielimisha jamii kupitia waandishi wa Habari mbalimbali Zanzibar.
“Tunaishauri wizara husika ya afya kudhibiti matumizi holela ya P2 kwa wasichana lakini, pia tunaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa afya ya uzazi kwa wasichana ili waepukame na matumizi mabaya ya P2” alisema kaimu mratibu wa tamwa pemba amina ahmed Mohammed
Kitengo cha afya ya uzazi na mtoto kimeeleza kuwa suala la afya ya uzazi sio jukumu la mtu mmoja pekee ambapo linaanza kwa mtu binafsi na jamii kwa ujumla, hivyo walezi na wazazi wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika kuwaelimisha watoto wao juu ya madhara ya kushiriki tendo la ndoa katika umri mdogo kwani husababisha madhara mengi ikiwepo saratani ya mlango wa kizazi.
“Iwapo tutashirikiana na jamii katika kuboresha afya ya uzazi kwa pamoja tutaepukana na ngono zembe hivyo hakutakua na sababu ya kutumia P2” alisema .
Matumizi ya P2 kwa wasichana wa Pemba ni changamoto ya kijamii na kiafya inayohitaji
kushughulikiwa kwa haraka. Elimu, uwazi na uwajibikaji ni silaha kuu za kulinda afya na heshima yawasichana wetu. Uzazi wa mpango ni haki, lakini unapaswa kufanyika kwa uelewa, usalama na
Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuhakikisha kizazi kijacho kinakuwa salama na chenye maarifa sahihi ya afya ya uzazi.na kujikinga namatumizi ya dawa hatari za p2
Fatma Shaame ambae sio jina lake sahihi alisema kuwa katika Kijiji chao uuzwaji wadawa hizo umekua ukiendelea kama ni bidhaa ya kawaida hali hio ikionesha kiashiria cha hatari kwa vizazi vyao
Ambapo aliongezea kusema kuwa suala hilo hufanywa kwa siri sana licha ya wazazi kuwachunguza Watoto wao lakini uingizwaji wa dawa hizo upo sambamba na kuiomba serekali kuweka udhibiti kwa vituo vyote vya uuzaji wad awa hizo kwani wafanya kazi wao ndio wahusika wa kuu wa usambazaji .
“ Mimi niiombe serekali kupipitia wizara husika kulifanyia kazi hili kwani wanaouza dawa hizi ni wao ambao wapo kwenye vituo vya afya ama maduka ya madawa , kuongeza umakini ili kukinusuru kizazi chetu” alisema Fatma.
Ni vyema jamii ikazingatia Matumizi ya P2 kwa wasichana wa Pemba ni changamoto inayohitaji hatua za haraka. Elimu, ushauri na uwajibikaji ni nguzo muhimu za kulinda afya na mustakabali wa mabinti wetu. Uzazi wa mpango ni haki ya kila mwanamke, lakini lazima utekelezwe kwa ufahamu, usalama na maadili.
0 Comments