WAANDISHI WA HABARI VIJANA ZANZIBAR WAPATIWA MBINU ZA KUIOKOA JAMII JUU TAARIFA ZA UONGO MITANDAONI.

Na-FATMA SULEIMAN 


Waandishi wahabari wachanga Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya kutambua taarifa sahihi katika kuelekea Uchanguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29/2025.

 Hayo yameelezwa na Mkurugenzi kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya wakati  akifungua mafunzo hayo kwa waandishi vijana kutoka Unguja na Pemba katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Mjini Unguja.

 Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwandaa Waandishi Habari vijana kutekeleza majukumu ya kihabari kwa weledi katika Dunia ya sasa iliyotawaliwa na matumzi mabaya ya ‘AKILI UNDE’ hivyo kuutumia katika kuondoa uongo uliopo katika jamii.

Aidha Mkurugenzi  amewasisitiza waandishi vijana kujifunza zaidi matumizi sahihi ya ‘AKILI UNDE’ ili kuhakikisha taarifa zinazosambazwa mitandaoni  kuuelewa usahihi wake.

“Waandishi vijana Miss information zimekua nyingi na endapo hazitasahihishwa jamii itaharibika na matumizi mazuri na mabaya Artificial Intelligence (AKILI UNDE) hivyo lengo la mafunzo haya kwenu ni kuona ni kwa namna gani mutaweza kutambua kati ya taarifa sahihi na zisizosahihi kupitia njia mbali mbali” Mkurugenzi alisema.

Akiwasilisha mada juu ya namna ya kuzitambua taarifa za Uongo na Ukweli wa Kihistoria Mkufunzi wa masuala ya Digitali Ephraim Muchemi, amewataka waandishi hao kutumia programu mbali mbali kama vile Google lens, Google Earth Google map nakadhalika ili ziweze kuwasaidia kupata ufafanuzi wa taarifa hizo.

“Kuna njia nyingi zinazoweza kuwasaidia katika kuzitambua taarifa za uongo na upotoshaji iwe maelezo, picha au hata video unaweza kuingiza sehemu ya maudhui hayo kwenye programu kama vile Google lens, Google Earth, True Caller nakadhalika na ukaweza kupata usahihi wa taarifa hizo” Mkufunzi Ephraim Muchemi alisema.

Kwa upande wake, Afisa programu kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi Tanzania Andrew Marawiti, amewataka waandishi hao kuendelea kuyafanyia kazi mafunzo hayo kwa vitendo  ili yaweze kuleta tija kwao na kwa na taifa kwa ujumla

“Kuwa kwenu hapa leo haikuwa Bahati mbaya tambueni kuwa mulikuwa wengi sana kwenye maombi ila nyinyi ndio tumeona munafaa zaidi kutokana na maelezo yenu kwenye maombi hivyo basi tunawaomba sana mukaendelee kuyatumia mafunzo haya kwa vitendo ili yaweze kuwajenga zaidi” alisema Afisa Adrew.

Akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Abdalla Mfaume, amesema katika zama hizi za maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, kumekuwa na ongezeko la habari za uongo na upotoshaji, hivyo aliwataka waandishi hao kuyafanyia kazi mafunzo hayo hususan katika kipindi hichi cha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.2025


“Katika kipindi hichi cha maendeleo ya sayansi na teknolojia changamoto za Habari za upotoshaji na uongo zimekuwa nyingi sana hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha munazitambua taarifa hizo ili zisiweze kuleta athari kwenu na taifa kwa ujumla” Alisema Mwenyekiti 

Baadhi ya Waandishi ambao wamepata nafasi ya kutoa neno ikiwemo kuushukuru Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuendelea kuyafanyia kazi hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.


"Kwanza nianze kwa kuwashukuru UTPC kwa mafunzo haya adhimu kwetu maana kwa kweli mitandaoni hali sio shwari na sisi Waandishi ndio wahanga wakubwa taarifa za uongo na upotoshaji kwa maana ya kutumia taarifa hizo" Salma Shaali Juma mwandishi kutoka Idara ya Uvuvi Zanzibar na Habari FM Radio 


Mafunzo hayo ya siku moja yalisyoshirikisha waandishi wa Habari Vijana kutoka Kisiwani Unguja na Pemba yameandaliwa na Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa ufadhili wa Netherlands (NL)

Post a Comment

0 Comments