MMOMONYOKO WA MAADILI KUWA TISHIO KWA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

NA -FATMA SULEIMAN-PEMBA 
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdalla Said, ametoa wito kwa taasisi zote zinazoshughulika na masuala ya ukatili wa kijinsia kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha hukumu zinatolewa kwa ufanisi na kupunguza ongezeko la matukio ya ukatili na udhalilishaji katika jamii. 
Ameyasema  hayo huko Gombani, Chakechake Pemba, katika warsha ya wadau kupitia mradi wa ZIQUE (Zanzibar Improving Equality basic Education) ilioandaliwa na wizara ya elimu kwa ufadhili wa benki ya dunia kupitia mpango kazi wa masuala ya ukatili wa kijinsia, unyonyaji, unyanyasaji wa kingono.
Aidha alisisitiza kuwa bila ushirikiano wa dhati, ushahidi hautokua wa kutosha, jambo ambalo litarudisha nyuma vita dhidi ya udhalilishaji ambapo aliwataka wazazi na walezi kudhibiti malezi ili kuepuka mmomonyoko wa maadili kwani suala la Ukatili wa Kijinsia (GBV) si la Wizara ya Elimu pekee, bali ni jukumu la kila mmoja.

 Mdhamini kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Moh'd Nassor Salim,  alieleza kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yanatokea kila siku na Serikali kupitia wizara ya elimu inaendeleza  juhudi za kutoa elimu, lakini bado watoto wanashambuliwa kwa kubebeshwa mimba hivyo kuwaomba wadau kuwasaidia kukabiliana na changamoto hio.
Nae Joyce Mgombele kutoka Wizara ya Elimu, amesema mradi huo wenye lengo la kujenga shule na vyoo ambapo kwa pemba skuli zitakazojengwa ni chuo cha kiuyu,wesha,miti ulaya na kengeja.
Alisema kuwa takwimu za kitaifa asilimia 40 ya wanawake wote wenye umri wa miaka 15-49 wamekubwa na ukatili wa kimwili asilimia 17 wamekubwa na ukatili wa Kingono hii ikionesha alama ya hatari juu ya matendo hayo.

Kwa upande wa wadau waliopatiwa mafunzo na  mradi huo wamesema watoto waliopitia vitendo vya unyanyasaji wanahitaji kupewa elimu ya ushauri nasaha katika kuwaepusha  kurejea tabia hizo, katika kuhakikisha wanaachana na mienendo mibaya.
" Ingawa sheria zipo, lakini  bado ni muhimu kushirikiana kwa pamoja  kuwapa elimu walioathirika ili waweze kusaidia wenzao na jamii kwa ujumla kubaki salama kwani watoto hawa hurejea vitendo hivyo mara kwa mara kutokana na kuathirika kwao"

"Kama mahkama ya mtoto hakuna kinachopatikana zaidi ya watoto kurejea udhalilishaji sheria ni mpya lakini zina udhaifu hivyo Lawama zinakuja kwetu sisi ofisi ya mahkama na ofisi ya Dpp kuonekana hatuna utendaji kazi"

Mradi huo ukiwa na lengo la kuwanusuru watoto na ukatili wa kijinsia ambapo waliopatiwa mafunzo ni wadau wote wanaojishughulisha na masuala ya udhalilishaji wakiwemo mahkama  dawati taasisi zisizo za kiserekali ikiwemo Tamwa ,Shijuwaza , SOS , Ofisi ya mufti, wizara ya elimu kupitia elimu mjumuishi kisiwani pemba.

Post a Comment

0 Comments