Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Mariam Mwinyi, ametoa wito kwa wanawake wa Kisiwa cha Pemba kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa dhati kwa kuhakikisha Dk. Hussein Ali Mwinyi anapata kura za kutosha katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na makundi mbalimbali ya wanawake katika mkutano mkubwa ulioandaliwa na UWT, uliofanyika kwenye uwanja wa kufurahishia watoto Tibirizi, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, Mama Mariam alisema kuwa kura hizo zitamwezesha Dk. Mwinyi kuendelea kuiongoza Zanzibar na kutekeleza ajenda ya maendeleo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Mama Mariam alieleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, chini ya uongozi wa Rais Dk. Hussein Mwinyi, Serikali ya Awamu ya Nane imefanikiwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020–2025, hususan katika sekta zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, ikiwemo elimu, afya, uwezeshaji wanawake, na miundombinu.
“Wanawake mmeshuhudia wenyewe jinsi Serikali ya CCM ilivyojitoa kuwahudumia kwa vitendo. Hii ni sababu tosha ya kuhakikisha tunamlinda na kumuunga mkono Dk. Hussein Mwinyi ili aendelee kutuletea maendeleo zaidi,” alisema Mama Mariam Mwinyi.
Aidha, aliwasihi wanawake kuwa mabalozi wa amani, mshikamano, na ushawishi katika jamii, kuhakikisha kwamba kila mwanamke anakuwa mstari wa mbele kushiriki uchaguzi kwa amani na kumpigia kura mgombea wa CCM.
Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kuimarisha kampeni zake kwa amani, mshikamano, na kwa kuzingatia maadili ya kisiasa, kikilenga kushinda kwa kishindo ili kuendelea kuwatumikia wananchi wa Zanzibar kwa ufanisi mkubwa.
Kwa Upande wa UWT,Makamu Mwenyekiti Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amewataia wanawake kujivunia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwanamke wa kwanza kupeperusha Bendera ya CCM kwa Nafasi ya Urais pamoja na kujivunia kazi kubwa za maendeleo alizozafanya katika kipindi cha Miaka minne,na itakapofika siku ya Uchaguzi kumpigia Kura pamoja na Dk. Mwinyi il maendeleo yapatikane kwa Miaka mitano ijayo.
0 Comments