MAENDELEO YALIYOLETWA NA DKT. SAMIA NA DK. MWINYI KURAHISISHA USHINDI WA CCM UCHAGUZI MKUU 2025-ZAINAB SHOMARI

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) ameeleza kuwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu utakuwa mwepesi kwa Chama Cha Mapinduzi kutokana na maendeleo makubwa nchini.
Maendeleo hayo ambayo yaliyoletwa na serekali ya CCM chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mgombea Urais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Makamu Zainab ameeleza kuwa Tanzania imejionea maendeleo makubwa ambayo yamekuwa yakihitajika na wananchi wakiweno wa Kisiwa cha Pemba.
Ameyasema hayo leo tarehe 02 Oktoba, 2025 alipokuwa akizindua Kampeni za CCM katika Jimbo la Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akiwaomba Kura wananchi wa Jimbo la Mtambwe kuchagua Viongozi wa CCM,Makamu Zainab amemuombea Kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi,Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtambwe Abas Ali Khamis ,Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Maryam Ali Rashid pamoja na Madiwani.

Post a Comment

0 Comments