TAMWA YAISHAURI JAMII KUUNGA MKONO TECHNOLOJIA KWA WATU WENYE ULEMAVU

 Imeandikwa na Tatu Juma Zanzibar



Jamii yapaswa kuungamkono ufanisi wa Teknolojia kwa watu wenye ulemavu.


Wito huo umetolewa na Afsa mipango na mawasiliano kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar Khairat Haji Ali  akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwao Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.


Amesema Teknologia kwa watu wenye ulemavu ni muhimu kwani nao ni miongoni mwa wanaadamu ambao wanastahiki kupata haki zao hivyo kila hatua yakimaendeleo ni lazima kuwashirikisha na wao.


Afsa Khairat ameendelea kwa kusema  kuwa inafahamika kwamba kuwepo Teknolojia nijambo muhimu katika Dunia hakuna haja yeyote ya kuwaacha nyuma kwani wanastahiki na wanauwezo mkubwa kuliko jamii invyowafikiria.


"Kwamfano hii teknolojia ya maandishi inayoitwa nukta nundu,hata katika maofisi pia kuna vifaaambavyo kama simu zina tecnolojia zitakazo wasaidia, hatuwezi kuwaacha nyuma hata kidogo kuanzia mashule Ofisi hata najamii kwaujumla" amesema Afsa Khairat


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wakalimani wa Lugha za alama Zanzibar Kheir Muhammed Simai akizungumza na habari hizi amesema.  Kuwa inatambulika kuwa sasa Dunia ipo katika ulimwengu wa Sayansi na Teknologia kwaiyo ameishauri Serikali pamoja na jamii kwa ujumla kuweza kutumia ipasavyo teknolojia ili kuweza kuwa na jamii jumuishi.


Hata hivyo ameiomba Serikali kupunguza ama kuondosha kabisa  kodi ya kuingizwa vifaa kwa watu wenye ulemavu kwani inafahamika kuwa asilimia kubwa ya vifaa hapa Zanzibari ni hafifu na inategemea vifaa kutoka nchi za nje.

"Kwamfano (lotion) ambazo wanatumia ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi (Maalbino) hapa kwetu Zanzibar hapana kwaiyo wanahitaji kupata nchi za nje kuingia hapa unakuta kwamba gharama zake mpaka zikamfika mtumiaji inakua ni gharama kubwa pamoja na vifaa vyengine"amesema Mkurugenzi Kheir.


Makala hii imebahatika kuzungumza na Mwenyekiti wa wa Asasi ya wahamasishaji elimu Zanzibar (AWEZA)ndugu Rajab Said Sisemi nae amesema kuwa ipo haja ya kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu hususan katika shuhuli za kimaendeleo ikiwemo kuwasimamia katika kuwaendeleza na elimu za juu.

"Katika Teknologia tunaweza kusema kwamba wanajitolea kwasababu wanahamu,lkn sijaona kwamba chuo hichi kimetengenezewa watu wenye ulemavu pekee all most tukasema kama Nkuruma,Mbweni,ikawa ipo kwamba watu wenye ulemavu njooni hapa kuna fani zote lakini tunashindikiza tu mkasome huku nahuku huwezi kujua changamoto gani wanakutana nazo"amesema Rajab Sisemi.


Akieleza kwa msisitizo amesema kuwa hatua ya kuwashirikisha na maendeleo ni jambo ambalo linawezekana kwani hata kipindi cha miaka ya nyuma wanawake walikuwa hawapewi kipaumbele lakini sasa wanawake wamewezeshwa  na wanafanya mengi ya maendeleo katika jamii.


Makala hii imebahatika kuzungumza na Mwenyekiti wa wanafunzi wenye ulemavu kutoka Chuo cha Taifa cha Zanzibar SUZA Nasri Salum Ali ambae anaulemavu waviungo nae ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuwapa msukumo wa kimaendeleo wanafunzi hususan wa elimu za juu  ili na wao wajisikie kuwa nguvuzao zinatumika nakuleta faida kwajamii.


Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar ni miongoni miongoni mwa Taasisi binafsi inayopambana katika kutetea haki za watu wenye ulemavu pia wamefanikiwa kuandaa miundombinu tofauti ili jamii iweze kufahamu kiundani haki za watu wenye ulemavu pamoja na kuhakikisha haki hizo zinatendeka ipasavyo.


Inafahamika ya kwamba katika kutatua changamoto za watu wenye ulemavu, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar SMZ imetaja hatua inazochukua ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushiriki wao katika ngazi za uamuzi kutoka asilimia mbili za sasa hadi tano ifikapo mwaka 2030.

MWISHO







Post a Comment

0 Comments