Imeandikwa na Tatu Juma Zanzibar
PAMOJA YOUTH INITIATIVE yatoa mafuzo kwa Asasi za kiraia pamoja na waandishi wa habari kuhusiana na usahihi wa uandishi wa habari za kijamii.
Hafla hiyo imeganyika katika ukumbi wa Skuli ya Tumekuja Kikwajuni Mjini Unguja.
Akizungumza na waandishi wa habari mkufunzi wa mafunzo hayo Mratibu wa mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu ndugu Suleiman Baitani amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa elimu kuhusu uandishi wa habari za kijamii pamoja na kuelewa sheria kwalengo la kutatua matatizo mbali mbaliyanayoikumba jamii pamoja na namna gani mwandishi anapata ulinzi katika kazi zake.
Amesema kuwa imegundulika kwamba kuna changamoto ya uandishi wa habari za kijamii ambazo zinagusa matukio ya wananchi hivyo kupitia mafunzo hayo itasaidia kuleta msukumo wa taswira sahihi kwakila habari inayotolewa.
Hata hivyo amesisitiza kuwa jamii iwe na desturi ya kuisoma katiba na sheria ili kujua wajibu pamoja na haki kwani kupitia hatua hii kuna uwezekano mkubwa wa kila raia kuweza kujifahamimu nakufuata muongozo sahihi.
Nae mkuu wa utawala na fedha wa Taasisi ya PAMOJA YOUTH INITIATIVE ndugu Mussa Mbwara akizungumza mwishoni mwa mafunzo hayo amesema kuwa kwamujibu wa teknolojia inavyokuwa nivyema kuitumia vyema mitandao yakijamii ili kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Hata hivyo amewapa matumaini makubwa wanamafunzo ikiwa watashirikiana pamoja ili kufikia lengo halisi la kuielimisha jamii nakupata mafanikio bora.
PAMOJA YOUTH INITIATIVE ni taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) inayofadhiliwa na vijana na kujikita katika kujenga uwezo na kuimarisha ushiriki wa vijana wa Zanzibar katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Ina dhamira ya kuwasaidia vijana kutambua na kutumia vipaji vyao, kushiriki katika uongozi, uchumi na jamii.
MWISHO
.jpg)
0 Comments