Umuhimu wa Lishe Bora kwa Makuzi ya Awali ya Mtoto


NA-Amina Ahmed 
Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya mtoto.
 Katika kipindi ambacho mtoto yupo chini ya umri wa  miaka mitano, mwili na akili hukua kwa kasi kubwa, na hatua hii huonekana  ukuaji wa mtoto katika maeneo mbali mbali , afya mwili, pamoja na akili. Tafiti za afya ya jamii zinaonyesha kuwa karibu nusu ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano hutokana na ukosefu wa lishe bora.
Lishe si suala la hiari bali ni uwekezaji wa maisha ya mtoto na jamii kwa ujumla.uwekezaji ambao humuandaalia kesho iliyo bora mtoto.
JEE kwanini  Lishe Bora ni Muhimu  kwa Makuzi ya Awali ya  Mtoto?
 Ukuaji wa Mwili
Protini, wanga, mafuta, vitamini na madini huchangia ukuaji wa mifupa, misuli na viungo.
Lishe bora huimarisha nguvu na uwezo wa mtoto kushiriki michezo na shughuli za kila siku.
 Maendeleo ya Akili
Virutubisho kama chuma, omega-3 na vitamini B huchangia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kujifunza.
Siku 1,000 za mwanzo (kutoka ujauzito hadi miaka miwili) ni kipindi cha dhahabu kwa maendeleo ya akili na kinga ya mwili.
 Kuimarisha Kinga ya Mwili
Vitamini A, C, D na madini kama zinc huimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa ya utotoni.
Lishe duni hudhoofisha kinga na kuongeza hatari ya maradhi ya mara kwa mara.

 Kuzuia Utapiamlo ambao ni Utapiamlo ni hali ya kiafya inayotokea pale mtu kukosa lishe bora ya kutosha na kupelekea :
Upungufu wa virutubishi (kama protini, vitamini, madini).
Lishe isiyo sahihi (kula vyakula visivyo na uwiano mzuri wa virutubishi).
Lishe kupita kiasi (kula chakula kingi kisicho na afya, kinachoweza kusababisha unene kupita kiasi na magonjwa yasiyoambukiza),utapiamlo ni tatizo la lishe linaloweza kuathiri ukuaji, afya, na uwezo wa mwili kufanya kazi vizuri jambo ambalo  husababisha kudumaa kwa ukuaji na matatizo yasiyorekebishika baadaye maishani.
Lishe sahihi husaidia kuepuka udumavu na upungufu wa damu kwa watoto.
Aina za Vyakula Bora kwa Watoto wa awali 

Inashauriwa kumuandalia chakula  cha  Asubuhi mtoto alie chini ya umri wa miaka miatano   kama vile ,Uji wa nafaka (mtama, ulezi au mahindi) uliopikwa kwa maziwa,Tunda moja kama ndizi, embe,papain a matunda mfano wa hayo.
Huku Mchana  aweze kula vyakula kama vile ,Wali au ugali pamoja na mboga za majani mchicha na nyenginezo),Kipande cha samaki au nyama ndogo dagaa  au supu ya mdagaa  samaki kulingana na uwezo  wa mlo wa siku. Pamoja na e cha juisi ya matunda safi.
na kwa wale  ambao wanautaratibu wa kula jioni  inashauriwa kwa mtoto aliechini ya umri wa miaka  5   kula vyakula kama vile Viazi vilivyochemshwa au mikate ya ngano,Mayai au dengu kwa protini pamoja na Mboga za rangi tofauti (karoti, nyanya, pilipili hoho).
Huku vitafunwa bora kwa mtoto vibaki kuwa ni 
Parachichi, karanga au maziwa ya mtindi,Matunda madogo kama chungwa au apple.
Ratiba hii inahakikisha mtoto anapata virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji wa mwili, akili pamoja na kinga ya mwili.
CHANGAMOTO KWA WALEZI NA WAZAZI 
Ukosefu wa uelewa: Wazazi wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu lishe sahihi.
Umaskini: Familia nyingi hukosa uwezo wa kupata vyakula vyenye virutubisho kamili.
Mila na desturi: Baadhi ya jamii hupuuza ulaji wa vyakula fulani kwa watoto, jambo linalozidisha utapiamlo.
Lishe bora kwa makuzi ya awali ya  mtoto ni nguzo ya afya na maendeleo ya maisha yake yote kwani inahakikisha ukuaji wa mwili, maendeleo ya akili, na kinga ya mwili. Familia, jamii na serikali zinapaswa kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula chenye virutubisho kamili. 
Kila sahani yenye lishe bora ni hatua ya kujenga kizazi chenye afya, chenye uwezo wa kujifunza na kuchangia maendeleo ya taifa.
# Mtoto Kwanza
2556859184
aminaahmedmoh@gmailcom
MD  digital

Post a Comment

0 Comments