Wananchi maeneo mbali mbali kisiwani Pemba wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru ifikapo tarehe 2 april mwaka 2026 katika uwanja wa gombani Chake chake Pemba.
Wito huo umetolewa na waziri wa wa nchi ofisi ya rais maendeleo ya vijana Tanzania Joel Arthur Nanauka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Katika ukumbi wa ZBC Mkoroshoni ikiwa zimebaki siku chache kuelekea uzinduzi wa tunu hiyo ya taifa iliyoasisiwa na baba wa Taifa Julius Nyerere .
Amesema kwa sasa maandalizi yote tayari yamekamilika hivyo ni vyema wananchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi huo ambao pamoja na mambo mengine unatarajia kuzindua majukwaa ya vijana maeneo mbali mbali utakapotembezwa mwenge huo wa uhuru.
0 Comments