Ameyasema hayo katika hafla ya ufunguzi wa kukabidhi mwenge wa uhuru kitaifa kwa vijana hao wa kukimbiza mwenge iliyofanyika Gombani Pemba kwa mwaka huu 2026
Aidha amewasisitiza wananchi Kulinda amani na umoja wakitaifa ulioasisiwa na viongozi kwa zaidi ya miaka 60 iliyopita kwani Tanzania inajulikana kuwa na amani kwa zaidi ya miaka hiyo.
Akitoa salamu za Mwenge Makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Mh Hemed Suleiman Abdallah amesema Tanzania inahitaji amani na maendeleo ambapo kupitia ufunguzi wa mwenge kunaakisi malengo ya Tanzania katika kuendeleza na kudumisha amani ya nchi.
Akizungumza waziri wa nchi ofisi ya raisi maendeleo ya vijana Tanzania Joel Arthur Nanauka amesema mwenge wa uhuru kitaifa wa mwaka 2026 utakimbizwa kwa mikoa 31 vitongoji 135 kwa siku 195 Tanzania ambapo maeneo ya kuzingatiwa ni pamoja ya Ukimwi, Rushwa , Malaria, Dawa za kulevya na Lishe bora.
0 Comments