Wilaya ya Chake Chake Wakabidhi Mwenge wa Uhuru kwa wilaya ya Mkoani kwa kishindo.


Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zimefikia hatua nyingine muhimu leo, aprili 3, 2026, baada ya wilaya ya Chake Chake  kukabidhi rasmi Mwenge huo kwa wilaya ya Mkoani katika  kiwanja cha Dodo Pujini 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Kaimu Mkuu wa wilaya ya Chake Abdalla Rashid Abdalla alisema kuwa  kwa wilaya ya  Chake Chake Mwenge wa Uhuru umepita katika miradi yote minne na programu mbali mbali ambapo thamani yake ni bilioni 19 milioni mianne na thelathini na tatu  ikiwemo elimu,miundombinu ya usafiri, afya na mradi wa vijana na kuridhishwa ubora wake.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki alipokea Mwenge huo kwa furaha na kuahidi kuendeleza kasi ya ukaguzi wa miradi  katika wilaya yake sambamba kuhamasisha wananchi juu ya mapambano dhidi ya Ukimwi,Afya na lishe,Mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na dawa za kulevya  kama ilivyoelekezwa na serikali.
Ambapo Jumla ya miradi 7 ya maendeleo inatarajiwa kufunguliwa, kukaguliwa pamoja na kuwekewa jiwe la msingi ikiwa ni  katika muendelezo wa  ukimbizaji wa mwenge wa uhuru kitaifa  katika wilaya ya mkoani   ambao ulianza ukimbizaji wake jana tarehe 2/04/2026


Mwenge wa Uhuru sasa utaanza kukimbizwa katika mkoa wa Mkoani  kwa siku moja kabla ya kuukabidhi mkoa unaofuata.

Post a Comment

0 Comments