Mku wa mbio za mwenge azindua barabara Jambangome aomba itunzwe.


NA-ARAFA MAKAME PEMBA.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Jambangome JCT yenye urefu wa kilomita 2.42 umezinduliwa rasmi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michel Mwang'onda ikiwa ni muendelezo waukimbizaji Mwenge wa uhuru kitaifa  nakuwaomba wananchi kuitunza barabara hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu nakuweza kunufaisha kizazi cha sasa nakinachofuata.

Aidha amesema endapo wananchi watatunza nakuithamini barabara itachochea maendeleo kwakuwa  serikali itaendelea kuleta miradi mingine pale inapothaminiwa nakulindwa vizuri.
 Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Afisa Mdhamini wizara ya ujenzi na  mawasiliano Ibrahim Saleh Juma , amesema mradi huo  unasimamiwa na Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na makampuni ya IRIS/ASER na MAWI, ukitekelezwa kwa teknolojia ya Chip Seal/Double Surface Dressing amabpo Ujenzi ulianza Julai 12, 2025 na unatarajiwa kukamilika mwezi huu, ukiwa na gharama ya Shilingi za Kitanzania bilioni tatu, milioni mia sita thelathini na nane, laki mbili kumi elfu mia tisa hamsini na senti hamsini na moja.
 shilingi bilioni 3.6 za Kitanzania.

Aidha, Afisa Mdhamini alieleza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 1 zimetumika kulipa fidia kwa wananchi 37 waliopisha mradi huo, huku mradi ukihusisha pia uwekaji wa mifereji ya maji, alama za barabarani pamoja na michoro maalum kwa ajili ya kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments