Watu 41 wamepatikanaa katika ukanda wa bahari ya hindi eneo la Kengeja Wilaya ya Mkoani Pemba baada ya chombo chao kupoteza mwelekeo kikielekea Comoro kisiwa cha Mayota kilichokwama siku 15 baharini amesem Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki.
Mkuu huyo amesema miongoni mwao ni wanaume 18 wanawake 23 watoto 11 uku mwanaume 1 na mtoto wamepoteza maisha walipokua wakikimbizwa Hospitali ya rufaa ya Abdalla zee Mkoani wote kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Akithibitisha kupokea wahanga hao, Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dk Aboud Khamis amesema hali zao zinaendelea kuimarika kadri muda unavyozidi kwenda.
Bi Miza ameongeza kua matukio kama haya huhusisha wavuvi baada ya chombo chao kupoteza mwelekeo au kumaliza mafuta na sio watu wanaokwenda kutafuta maisha sehemu nyengine.
0 Comments