Kojani walia na ukosefu wa elimu ya hedhi salama.


Elimu ya hedhi salama bado mashuleni.
NA KHAULAT SULEIMAN-PEMBA.


 hedhi ni mchakato wa homoni unaofanyika mara moja kwa mwezi. Mwanamke wa kawaida atapata vipindi vipatavyo 450 katika maisha yake.
Kwa baadhi ya wanawake, mzunguko wao wa hedhi huanza na kuishia kwa wakati mmoja kila mwezi, lakini kwa wanawake wengine, matatizo ya hedhi yanaweza kusababisha usumbufu katika maisha yao ya kila siku. 
Katika baadhi ya matatizo haya, dalili za kimwili na kihisia kama vile maumivu, kutokwa na damu nyingi, na mabadiliko ya hisia yanaweza kufanya shughuli za kila siku kama vile kuhudhuria shule au kazi zisiwezekane, na pia inaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa zaidi la kiafya. 


Maumivu ya Hedhi
Maumivu ya hedhi yanayoambatana na hedhi hujulikana kama dysmenorrhea . 
Maumivu, kwa kawaida katika eneo la fupanyonga, ndiyo tatizo la kawaida ambalo wanawake hupata wakati wa hedhi zao. Ingawa dawa ya maumivu ya bila agizo la daktari kwa kawaida inaweza kusaidia, kuna chaguzi zingine za matibabu zinazopatikana kulingana na ukali na chanzo cha maumivu.
 Dysmenorrhea kwa kawaida hugawanywa katika kategoria mbili. Dysmenorrhea ya msingi ni ya kawaida zaidi na husababishwa na mikazo kwenye uterasi. Dysmenorrhea ya pili kwa kawaida husababishwa na tatizo maalum la kiafya kama vile endometriosis au uvimbe wa ovari.
Hapa tunaona sasa jinsi gani wanafunzi wanavoshindwa kuendelea na masomo pamoja na kupatwa na maumivu.
Mwanafunzi Fatma Said mkaazi wa Kojani wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba amesema kuwa,ukosefu wa elimu wa hedhi salama huchochea utoro shuleni na kukosa vihifadhio vya kujihifadh hali inayowafanya kukosa hamu hata katika masomo yao.
Naye mwalimu Mtumwa Faki Said amesema zaidi ya wanafunzi 2000 katika skuli hiyo hua hapo katika kipindi cha balekhe na hukosa uhifadhi wa kipindi hicho wengi hawana elimu na matumizi ya taulo hawana mna sio wote hutumia laki tunachukuwa hatua za kuwa elimu pamoja na kuondokana na matumizi yasiyorafiki ya taulo ikiwemo matambara yasiyorafiki.
"Mwanafunzi anaweza akaja skuli harufu unaiskia kutokana na kutojihifadhi vizuri au matambara kutokauka na kuvaa hivo hvo hii humfanya mwanafunzi mwenye kutokua imara na kukosa hamu ya kusoma"alisema.
Vipindi Visivyo vya Kawaida
Hedhi zisizo za kawaida na mizunguko ya hedhi ambayo huanza siku 24 au chini ya hapo baada ya kuisha kwa hedhi ya mwisho au ikiwa mzunguko unaanza siku 38 baada ya kuisha kwa hedhi ya mwisho.
 Hedhi zisizo za kawaida pia hufafanuliwa kama tofauti katika urefu wa mzunguko wa hedhi. Ingawa ni kawaida kwa hedhi zisizo za kawaida kutokea kwa wasichana vijana na wanawake walio katika kipindi cha kukoma hedhi ikiwa unapata mzunguko usio wa kawaida wa hedhi nje ya viwango hivi vya umri.
Mwalimu mkuu wa skuli ya Utaani Siti Faki Ali amesema wanafunzi wanapokua na elimu hedhi salama husaidia kujihifadhi wao wenyewe na kuendelea na shughuli zao za kila siku tafauti na wanapokosa elimu .
"Sisi katika dakhalia yetu ya Utaani na chasas wanafunzi wengi hupewa elimu ya hedhi salama na taulo za kujihifadhia".alisema.
Kutokwa na damu nyingi
Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kunaweza kusababisha usumbufu mkubwa katika maisha ya kila siku.
Unatakiwa kubadilisha yako kila baada ya saa moja au mbili, kutoa damu iliyoganda zaidi ya robo, au kuwa na hedhi inayodumu zaidi ya siku nane, kutokwa na damu kwako kunaweza kuwa dalili ya matatizo mengine ya kiafya.

AFISA ELIMU WILAYA.
Kaimu Afisa elimu wilaya ya wete Badyura Suleiman Abdallah elimu amesema wao wana jukumu la kuhakikisha katika maskuli wanapewa elimu laki pia na kutoa pendi kwa kila skuli zenye dakhalia ili kuwasaidia watoto wa kike katika kipindi hicho kigumu wanachokuwa nacho.
"Wengine hawanauwezo wa kununua hii husaidia kwa kiasi kikubwa na hata kuwafanya kuwa safi katika kipindi hicho tafauti na matumizi mengine wanayotumia ili kujihifadhi".alisema.

Kutokwa na damu Isiyo ya Kawaida
Kutokwa na damu isiyo ya kawaida hujulikana kwa kutokwa na damu ambayo hutokea nje ya mzunguko wako wa hedhi. Mifano ya kutokwa na damu isiyo ya kawaida ni pamoja na kutokwa na damu mara kwa mara baada ya ngono, na kuonekana kati ya mizunguko. Sababu zinazowezekana za kutokwa na damu isiyo ya kawaida huanzia mabadiliko ya homoni hadi saratani fulani, kwa hivyo hakikisha unamuona daktari wako kubaini ni nini kinaweza kuwa hali ya msingi ya kutokwa na damu isiyo ya kawaida.

Kukosa Hedhi
Wanawake wanapokosa hedhi, wazo la kwanza la wanawake wengi huenda moja kwa moja kwenye ujauzito, lakini kuna sababu nyingi tofauti kwa nini mzunguko wa hedhi unaweza kuachwa. 
Wakati hedhi haitokei kwa zaidi ya miezi mitatu mfululizo, au ikiwa hedhi haianzi kabla ya umri wa miaka 15, hali inayoitwa amenorrhea inaweza kuwa sababu ya kutokuwepo kwa hedhi kwa muda mrefu. 
Wakati amenorrhea inatokea nje ya ujauzito au kunyonyesha, inaweza kuonyesha kwamba ovari zako zimeacha kutoa kiasi cha kawaida cha estrojeni, ambacho kinaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi ya kiafya katika siku zijazo. 
TAKWIMU.
Takwimu zinaonesha kwamba takriban wanawake milion 13.7 nchini wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 49 ambao kimsingi huwezi kupata hedhi kila siku,hivyo jamii inatakiwa kuweka mazingira wezeshi kwa mwanamke ili apate hedhi salama "Amesema mhe. Mtahengerwa.
MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni khatib Yahya katika ziara zake maeno ya visiwani aliwataka wanafunzi husasa ni wakike kuwa makini katika masomo yao licha ya changamoto mbaki mbali wanazopitia ikiwemo katika kipindi cha hedhi na kuwataka kuwa wasafi katika kipindi hicho.
Aidha aliwataka wanafunzi hao kutokushawishika na wanaume kwa kutokana na hali yao waliyokuwepo kwa kuhadaliwa huduma.
Mashirika mbali mbali wanaohusika na utowaji wa misada ya uhidhi wa watoto wa kike kwa kuwapatia taulo ikiwemo Asma mwinyi Foundation na Mwanamke Inisitive Founation bado ipo haja kwa wanafunzi wa vijiji kuweza kuwatia elimu na misaaasa mbali mbali iki kupunguza wimbi kibwa na wanawake ambao hawana elimu na wanashindwa kujihifadhi.
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments