Ujasimali ulivyopunguza udhalilishaji hususani kwa wanawake.

NA KHAULAT USLEIMAN, PEMBA.
Ujasiriamali umepunguza kwa kiasi kikubwa udhalishaji wa wanawake kwa kuwezeshwa kiuchumi kupitia miradi na mikopo mbali mbali inayotolewa serikalini ili kuweza kujikwamua kiuchumi.Hatua hii inafanikiwa kupitia kuongeza uzalishaji mali, kutoa ajira kwa vijana wengi kupitia sekta binafsi, kukuza kipato binafsi, na kupunguza mzigo kwa serikali.
Mikakati mikuu inayofanya ujasiriamali uwe suluhisho ni pamoja na:Kujiajiri badala ya kuajiriwa: wanawake wengi sasa wanaanzisha biashara zao mara baada ya masomo kuachwa na kujiona ameachiwa kujukumu kubwa la ulezi hivo huanzisha biashara zao.

Ukuaji wa sekta binafsi,Biashara ndogo zinazofunguliwa zinahitaji wafanyakazi wengine ili kukua Kupunguza mzigo wa serikali.
Serikali haihitajiki kuajiri kila mtu kwa wakati mmoja,Kuongezeka kwa kipato ,wananchi wanajiongezea kipato chao kupitia biashara na uzalishaji.
Uwezeshaji wa mikopo Serikali inatoa mikopo nafuu kuongeza mtaji kwa wajasiriamali ili kukuza pato lao kiuchumi.
ZEEA ni miongoni wa sekta iliyoundwa na rais wa Zanzibar kwa lengo la kuwawezesha wajasimali kupitia mikopo mbali mbali.
MRATIBU ZEEA.
Mratibu wa ofisi ya uwekezaji wananchi kiuchumi Zanzibar ZEEA Haji Mohamed Haji amesema miongoni mwa mwajukumu yao ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii katika suala zima la kijikwamua kiuchumi na kuwapatia mikopo .
‘’ipo mikopo mbali mbali ikiwemo Dk. Mwinyi busting fund ambao kwa asilimia 80 imelenga wanawake billion 5 laki kwa sasa imebakia billion 2.5’f 42 budhabi.karafuu skim.
Lile lengo la rais wa zanzibar katika kuwainua wajasimali linasaidia kwa kiasi kikubwa husasa ni wanawake kwani wanawake walio wengi wa sasa hivi wamejikita katika ujasimali kwa bidha tofauti na hujitangaza kupitia mitandao ya kijamiii ikiwemo facebook ,twittter XI na Istagram Tiktok.

Elimu inapaswa kuzingatia kutoa ufahamu wa kina kuhusu fursa za ajira, zinazopatikana kwenye masoko na sehemu mbali mbali,hii inaweza kujumuisha sekta mbalimbali kama kilimo, ufugaji, na ubunifu. watu wengi wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kujiajiri wenyewe na kuwa wabunifu katika kuanzisha biashara zao.

MWANAMKE

Meiya Mbarouk ambaye ni mjasimali aliyeza kuwajiri na wanawake wenzake kwajili ya kuweza kujitaptia kipato Pamoja na kutoa mafunzo kwa wanmawake wenzake wajasimali.
Meiya ni mama mkaazi wa chasasa Wete na pia ni mbunifu katika harakati za ujasirimali alieleza kuwa kupitia ujasimali aliweza kujiajiri na kuachana na dhana ya kusubiri ajira kutoaka serikalini na kuona ni namna gani anatafuta soko la kibiashara ndani na njee ya nchi kwa kujitangaza kupitia mitandao ya kijamii.
‘’mafunzo mbali mbali Napata naenda katika mikoa inapotokezea maonyesho hii inanisaidia kupata huduma zangu na pia kuacha kutemea kuomba ujasimali unasaidia mwanammke kujikinga na udhalilishaji.”alieleza
Asilimia 78 ya kazi yangu ya ujasimali imenifanya kuweza kujikwamua kiuchumi na kuapambana kama mwanamke katika harakati.
Fatma hamadi mkaazi mzambarauni ambaye ni mjasimali alisema kuwa kazi hiyo ilifanya kuwa mwana haraki na kuacha kabisa suala la kutemea ndugu katika mahitaji yake ya msingi.
Huu ni Ushahidi tosha kuonesha kwa ujasimali unavowasaidia wanawake kuepukana na maswala ya udhalilishaji kutokana na shuguli zao wanazofanya.
MTAKWIMU
Katika bajet ya Zanzibar ya mwaka wa fedha 2026/2027 ya kiasi cha shilling trillion 8.5 serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZimeweka mikakati maalum kwajili ya wajasimali na wafanya biashra wadogo wadogo na wa kati (SMEs)mikakaiti hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha ustahamilivu wa uchumi kupitia mapato ya ndani na mageuzi ya kidigitali.
Serikali inaweza kuanzisha programu kama ilivyo Mwanza Academy for Women Entrepreneurs (AWE), na kuhakikisha kuwa zinawafikia wanawake na vijana wa kote nchini. 
 
Programu hizi zinaweza kutoa elimu ya vitendo na mikopo ili kuwawezesha wanawake na vijana kuanzisha biashara zao ,Kuweka mkazo kwenye usawa wa kodi kwa wafanyabiashara wa kuanzia kunaweza kuwa njia nyingine ya kuhakikisha vijana wanapata nafasi nzuri katika ulimwengu wa biashara.
Kwa kutoa elimu, kuendeleza vipaji, na kutoa fursa za kifedha, serikali inaweza kusaidia kubadilisha mtazamo wa vijana kutoka kuomba ajira kuwa waanzilishi wa biashara na wachangiaji muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Hatua hizi ni muhimu kujenga jumuia yenye nguvu na kuongeza uchumi wa nchi.
Mwanamke ambaye sio mjasimali Hasina said mkaazi waa madenjani ambaye ni mjane hana kazi n ani mama wa familia alieleza kuwa.
“mie sina shemu ya kunipatia kipato mpaka nimsubiri aliyekua mume wangu alete chaku cha wanawe ndio n amie nipate pesa laki ingekuwa nipo na kazi yangu nisingehangaika mna sabuni inanishindwa nahisi na dhalilika na Watoto.’’alisema.
Licha cha akina mama kuwa ni vichwa vya familia laki kwa Maisha ya hivi sasa asilimia 80 akina mama wananafasi kubwa katika kila Nyanja za kijamii na hata za kiserikali hivyo bado ipo haja ya akina mama kuongeza kasi katika harakati za ubunifu na uzalishaji wa kiuchumi.
TAMWA 
Tamwa ni wadau muhimu katika kupambana na maswala ya udhalilishaji kwa kutoa mafunzo kwa wandishi wa Habari ili kuona ni mna gani matendo hayo yanaweza kupungua na kuondoka kabisa.
Afisa mradi wa Pamoja wa kupambana na maswala ya udhalilishai Zanzibar Asya Hakim Makame amesema mradi huo umelenga kuibu maswala ya udhalilisha katika sehemu zisizo rasmi ili kuona ni kwa namna gani serikali na tasisi binafsi zinawekeza katika kupambana na maswala hayo.
MWISHO.

Post a Comment

0 Comments