Kuelekea Siku ya mtoto wa kike ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 11 October ya kila Mwaka
karibu kuisoma makala hiii...
Mtoto ni kila binaadamu ambae yupo chini ya umri wa miaka
Kumi na nane (18).
Hivyo kwa mujibu wa sheria tofauti za mtoto kama vile sheria
ya mtoto ya mwaka 2009 imeelezea
bayana masuala mengi ya kitaifa kuhusu haki na ulinzi wake
kwani sheria hiyo imechukua mikataba
na makubaliano mbalimbali ya Kimataifa yanayohusu haki za
watoto sambamba na kulenga
kuimarisha haki za watoto zikiwemo haki ya kupatiwa mahitaji
ya msingi kama chakula,malazi
,mavazi,matibabu,chanjo,elimu,pamoja na haki ya kucheza na
kuburudika...
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la SNVS
Netherlands Development Pamoja na Tanzania
Water and Sanitation Network (TAWASANET) katika halmashauri
za Sengerema,Mufindi,Chato,na
Temeke ulionesha kuwa asilimia 48 ya wanafunzi wa kike hukosa
masomo wanapokua kwenye hedhi
huku asilimia 78 ya waliohojiwa walisema kipindi cha hedhi
huathiri uwezo wao wa kujifunza.
Utafiti huo unatuonesha ni kwa jinsi gani mtoto wa kike hata
akikua na akiyafikia mafanikio basi kazi
kaifanya kwelikweli! kwasababu hata kimaumbile inaonekana
wazi kwamba Mtoto wa kike kila siku
yeye lazima atapitia changamoto tu!
mfano tujiulize tu kwa siku mtoto wa kike amejiandaa kuvaa
sare zake aende masomoni je?
bodaboda ngapi zitamuita kwa ajili ya msaada wa lifti? Je ni
wauza chipsi wangapi watamhadaa? Na
Je! Wauzaduka wangapi watajifanya kuongea nae sana! Ilimradi
tu kwa vile yeye ni wakike?
Unakuta kila siku hajaitwa asubuhi alipokwenda Skuli basi
kaitwa jioni ilimradi inasikitisha mtoto
wa kike ni yeye na Changamoto za njiani apitamo hata akifika
huko Skuli basi yuhoi !
lakini wakati huo huo ikumbukwe tu kwamba yupo na mtoto wa
kiume ukute changamoto hazipati
nyingi kama anazopitia huyu mtoto wa kike!
Suala la kujiuliza tena ni je ? Wazazi ama walezi
wanazingatia hilo? Haizidi mtoto wa kike ndio hanza
huachiliwa tu huru kutembea peke yake njiani, pasi na
kuzingatiwa usalama wake humo
anamotembea akiwa peke yake na kwa kutokana na mfano wa
changamoto hio ndio maana
hutokezea matukio mengi ya vitendo vya Udhalilishaji.
Nilizungumza na mtoto Fatma Ali ( Jina sio sahihi) kupitia
makala hii aliniambia kama ifuatavyo
kupitia Nukuu yake..
“Mimi darasani sisomi kwa amani, namuelewa Mwalimu
anavyonifundisha lakini tangu wanafunzi
wenzangu walipofahamu kuwa nilibakwa basi sina amani kila
nipitapo huwa naonyeshewa mimi tu
Vidole yule! Yule! Mtaani kwetu ndo usiseme mpaka nabadilisha
njia ili nikwepe changamoto za
kuendelea kudhalilishwa lakini bado"
Kadhalika wengine hupitia katika malezi ya baba tu ilihali
wao ni watoto wa kike! Je ?:hatuoni
kwamba hiyo ni changamoto pia kwa Mtoto wa kike? Labda kuna
maswali ya kujiuliza kwa mara
nyengine ili tuzinduke jinsi mtoto wa kike alivyohatarini
kimakuzi.
Nae Bimkubwa Muhammed mzazi mwenye watoto Sita Mkaazi wa
Fuoni Mambo sasa Zanzibar
alisema wababa kazi yao Kubwa ni kulaumu tu katika
malezi,unakuta husubiria mtoto wa kike
ateleze tu ndipo wabwate! Ndipo anasema alikuwa akijiuliza
kwani huyu mtoto wa kike ni wa mama
peke yake?
Na Je ?Kwa baba ambae anamlea binti wa kike peke yake pasi na
kuwashirikisha wengine hata
mashangazi! Huu uthubutu hasa wa kuongea nae mambo nyeti
utatokezea wapi ?
Kuna wazazi wajasiri sihaba wanamoyo wa kulea pande za Jinsi
zote bila ya kujali hatakama mtoto
wake ni wa kike atamueleza tu ukweli wote ilihali yeye ni
mwanaume na hivyohivyo kwa mtoto wa
kiume ilihali mzazi ni Mwanamke.
“Kuna msemo unasema Sikio halizidi kichwa hivyo tutake
tusitake kuna Uhusiano mkubwa wa
karibu wa kimalezi uliopo kati ya Mzazi wa kike na Mtoto wa
kike siku zote Mama yupo juu tu
kimalezi! tofauti na yule mzazi wa Kiume kimalezi kwa mtoto
wa kike”
Alizungumza nami kupitia Makala hii Bi Maryam Rashid ambae ni
mzazi wa watoto wanne, wote ni
Wanawake yeye ni mkaazi wa kisiwandui Zanzibar kwa kuniambia
kupitia nukuu yake.
“Kumlea mtoto wa kike ni Jukumu la kila mmoja tatizo lililopo
ni kwamba wanaume ni wategevu
kimalezi ,mzigo mkubwa huwaachia Wanawake sasa Mwanamke
atayafanikisha mangapi? Wao si
wakuuliza kabisa kuhusu maendeleo ya mabadiliko ya mtoto wa
kike wanachokijua wao ni kulaumu
tu! Alisema kwa masikitiko Bi Maryam
Aliendelea kwa kusema Kuna mambo mtoto wa kike ambae
analelewa na baba tu hatokuwa na
uthubutu wa Kuyazungumza ama kusema kwa baba yake na
inategemea ila wengi wanaolelewa na
baba tu! huwa wasiri wa kuelezea changamoto zao na mwisho wa
siku balaa huwakumba watoto
wa kike! Ndo pale mimba za kushtukiza hujiri kwao kumbe
hawakuwa wawazi wa kukaa na wazazi
ama walezi wao kwa ukaribu na kuwaambia.
Kwa Ushahidi wa uthubutu kwamba mtoto wa kike sio rahisi kuwa
muwazi kwa kulelewa na baba tu
! hebu tujiulize tena!
Je? Mtoto wa kike anaweza kumuambia baba yake kwamba njiani
kanifuatilia fulani? Ama Baba
naomba pesa nikanunue pedi? Au baba nimekamatwa sehemu nyeti
leo na wahuni huko njiani?
Kiukweli majibu ya masuala hayo hurejea pale pale kwamba Hata
Mtoto wa kike akikua basi Yuhoi!
Ni ukweli usiopingika kuwa Jukumu la Malezi ya mtoto wa kike
ni la baba na mama na ni vyema
kushirikiana katika malezi kwani Nguvu ya pamoja katika
malezi ni muarubaini wa kutatua
changamoto za malezi kwa watoto...
0 Comments