Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,
Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Seif Shaaban Mwinyi, amewataka watendaji wa
taasisi zinazojishughulisha na hifadhi za misitu na ukaguzi wa mizigo bandarini
na viwanja vya ndege kuyatumia mafunzo waliyopewa ili lengo la kudhibiti
biashara haramu ya viumbe hai adimu na walio hatarini kutoweka lifikiwe.
Akizungumza wakati akifunga
mafunzo ya siku tatu juu ya kuongeza uwezo katika kupambana na biashara ya
wanyama na miti hai adimu katika ukumbi wa hoteli ya Verde Mtoni.
alisema mafunzo hayo
yatawasaidia katika kuongeza ufanisi katika kazi zao ili kunusuru biashara
haramu isiweze kuingia nchini.
Aidha aliwataka watendaji
wanaoshughulika katika Ukaguzi wa magari ya Mizigo kua makini katika mizigo ili
bidhaa hizo za Wanyama pori na miti iweze kudhibitiwa.
Alisema kwa mujibu wa sheria
zilizopo katika shughuli za uhifadhi wa misitu hairuhusiwi kwa mtu yeyote
kusafirisha bidhaa zinazotokana na wanyama au miti iliyo hatarini kutoweka.
"Nataka niwaambie hasa kwa
wale watendaji waliopo katika bandari na Uwanja Wa Ndege kuwa makini katika
Kukagua bidhaa, hivyo tumaini langu baada ya Kumaliza mafunzo haya Mtakua
Mstari wa Mbele katika kupambana na wale wanaoingiza na kutoa Bidhaa kinyume na
sheria", alisema Seif.
Hata hivyo alisema Kila
kilichopo duniani kina Faida kubwa na kimeletwa duniani ili kisaidie hivyo
hakuna budi kuzitunza rasilimali hizo kwa kua zina umuhimu mkubwa kwa faida ya
kimazingira, kiuchumi na kijamii.
Mapema Kaimu Mkurugenzi wa Idara
ya Misitu, Abass Juma Mzee, alieleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu ikizingatiwa
kuwa Zanzibar ni kitovu cha biashara chenye milango mingi ya kuingia na kutokea
kwa bidhaa zikiwemo bandari bubu hivyo anaamini mafunzo waliyopewa yataimarisha
umakini kwenye utendaji kazi wao.
Kwa Upande wake Mkaguzi wa
Bidhaa Bandarini, Mohamed Abass Abdalla, akizungumza kwa niaba ya washiriki
wengine, alishukuru kuwa miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo kwani
yamewaongezea weledi utakaowasaidia
0 Comments