Imeandikwa na Fatma Abrahman – Pemba
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amesema
Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar linatarajia mabadiliko makubwa ya
kiutendaji unaozingatia utoaji wa haki kwa wananchi kufuatia mafunzo ya mara
kwa mara yanayotolewa kwa Askari kuhusiana na haki za binaadamu.
Akizungumza katika mafunzo ya haki za binaadamu kwa Askari wa
Polisi Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba huko Madungu Wilaya ya Chake chake ameeleza
kuwa, ili haki zipatikane kwa wadau wote
wa haki Jinai hawana budi kubadilika katika utendaji kwa kuzingatia utoaji wa haki.
"Baada ya mafunzo haya nategemea mabadiliko ya
kiutendaji kwahiyo malalamiko ya watu
kunyimwa haki zao kwenye vituo vya polisi yatapungua mana hatuwezi kusema
yatamalizika kwani binaadam hakuna mkamilifu "alisema Kamishna .
“ niviombe vyombo vinavyotengeneza mfumo wa haki jinai kushirikiana
pamoja na Polisi kwa sababu wananchi wanataka haki sawa kwa wote, tusiwe
tunazizungusha haki za watu , tuungane na kuwapa haki wananchi ili kuiweka nchi yetu katika Hali ya usalama
na amani " alisema Kamishna
Nae Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Mhe Jaji Mshibe Bakari
amehimiza kuchukuliwa hatua kwa makosa
madogo madogo ya uvunjivu wa haki za binadamu kwani kupuzwa kwa makosa hayo kunaweza kukasababisha madhara
makubwa hapo baadae.
"Lengo ni kuitaka jamii iishi kwa salama, kusiwe na
manung'uniko yasio kuwa ya lazima au kupelekea mambo ambayo ya uvunjifu wa
amani kwani haya makosa mafodo madogo ya uvunjifu ndio hupelekea madhara
makubwa hapo baadae hivyo umakini na usawa unahitajika kwa Hali na Mali
tuwajibike " alisema jaji .
Mkurugezi wa Taasisi ya kupambana na Changamoto za Vijana
Zanzibar (ZAFAYCO) ABdalla Abeid amesema Jumuia hiyo imejikita kutoa mafunzo ya
haki za Binaadamu kwa askari wa Jeshi la Polisi
ili kuzidi kufanya kazi zao kwa misingi ya sheria ili kujiepusha na
malalamiko ya jamii dhidi yao.
Nao askari wa mikoa yote miwili ya Pemba wameeleza kuwa,
wataendelea kutekeleza majukumu yao kwaajili ya kulinda haki za raia katika
ustawi wa jamii ambayo wanaisimamia.
0 Comments