Hapa ni maeneo ya Wawi kusini Pemba, harakati za wanajamii zikiendelea kama kawaida .Katika picha hii kuna vingi vinavyoonekana lakini moja ya vitu hivyo ni kuwa, bado miundombinu ya barabara katika baadhi ya maeneo kisiwani Pemba ni dhaifu hasa hii ya kuanzia machomane hadi Wawi, ni wajibu wa wahusika kuliangalia hili. Aidha, kwa vyombo vya moto barabarani bado kuna madereva ambayo hawajawa na uthubutu wa kuacha kupakia abiria katika idadi maalum inayotakiwa, kama picha inavyojieleza (Picha na Fatma Abrahman )
Camera ya Zenji Update leo hii imeyanasa mazingira haya, ambayo inaonesha jamii ya hapa Kojani wapo wanaopata shida sana ya kukosa huduma ya maji safi na salama kwa matumizi ya kawaida, kidogo tulipata kuwauliza, na sauti zao zilisikika wanashida ya maji, ni wakati kwa mamlaka,wahisani na wadau wa maendeleo kuelekea Kojani kwa lengo la kwenda kuwatatulia kadhia hii.Picha na Fatma Abrahma.
Huu ni muonekano wa mji wa Chakechake Pemba. Kisiwa cha Pemba rasmi kimeanza kupokea rasharasha za mvua za hapa na pale, unapata ladha gani unapoona mazingira haya ? Picha na Fatma Abrahman.
0 Comments