Imeandikwa na Fatma Abrahman – Pemba
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Khamis
Abdullah Said amewataka Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kojani kusoma kwa bidii
ili waweze kufaulu kwa viwango vya juu.
Nasaha hizo amezitoa wakati alipotembelea Skuli ya Sekondari Kojani na Kuangalia harakati za Ufundishaji na mazingira halisi katika Skuli hiyo.
Amewataka Wanafunzi hao kudumisha nidhamu ili waweze
kufanikiwa katika kufikia malengo waliyojiwekea katika Maisha yao.
Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga
Skuli ya kisasa katika kisiwa Cha kojani ili Wanafunzi waweze kusoma katika
mazingira mazuri.
Aidha amesema Wizara ya Elimu inatarajia kuanzisha somo la
uvuvi katika Skuli ya kojani ili kuwaandaa Wanafunzi katika fani inayoendana na
mazingira yao.
Mwalimu Mkuu Skuli ya Sekondari Kojani Nd. Khamis Amour
Khamis amesema ziara hiyo ya Katibu Mkuu katika Skuli yake imekuja katika
wakati muafaka kuelekea Mitihani ya Kitaifa hivyo itaongeza Ari na hamasa kwa
Wanafunzi katika kujiandaa na Mitihani hiyo.
Amesema katika Mitihani ya majaribio kiwilaya ni Wanafunzi 5
tu ambao walipata divisheni zero hivyo ziara hiyo itasaidia kuamsha Ari ya
kufuta zero hizo,
Kwa Upande wao Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kojani
wamesema Wamefarijika Sana baada ya kupokea nasaha za Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Wameahidi kuongeza jitihada katika kujiandaa na Mitihani.
0 Comments